Historia ya Vita vya Kagera na Ushindi kwa Majeshi ya Tanzania

KUTOKANA na umuhimu wa Historia ya Ushindi kwa Majeshi ya Tanzania dhidi ya Majeshi ya Uvamizi ya Nduli Iddi Amin Dadaa wa Uganda. Nikiwa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Tanzania, nawajibika kurudia sehemu ya Historia ya Vita vya Kagera ili kuweka mtiririko mzuri wa historia hii ambayo ni muhimu sana kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Hakuna Mtanzania asiyefahamu kuwa mnamo mwaka 1971 Nduli Iddi Amin Daa alitwaa madaraka ya nchi ya Uganda kwa mabavu na kuitawala nchi hiyo Kijeshi hadi mwa 1978 alipoyaamru Majeshi yake kuvamia Ardhi ya Tanzania, sehemu ya Mto Kagera, katika mkoa wa Ziwa Magharibi, ambao sasa ni mkoa wa Kagera.

Majeshi hayo ya uvamizi kutoka Uganda yaliua Watanzania hovyo,kuiba mali nyingi na kuzipeleka Uganda. Kutokana na uvamizi huo, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania wakati huo akiwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliutangazia Umma kuwa, Taifa lina kazi moja nayo ni kumpiga Amin na kumuondoa kwenye Ardhi ya Tanzania.




Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU