SIMBA YAIBAMIZA AFRICAN LYON 3-1

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam.imeanza Ligi Kuu mzunguko wa pili kwa kishindo baada ya kuibamiza Afrika Lyon pia ya Dar es Salaam kwa mabao 3-1, katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo.

Ramadhan Chombo 'Redondo' alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake bao la kuongoza baada ya beki wa kati wa Afrika Lyon Ibrahim Job kuzembea kuokoa mpira uliopigwa na Mrisho Ngasa wa Simba na kumkuta mfungaji.

Kuingia kwa bao hili kulisababisha hofu kwa mabeki wa Lyon ambao walipoteana na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao, lakini kipa wa timu hiyo. Abdul Seif alisimama imara kuokoa hatari zilizoelekezwa langoni kwake. Pamoja na umahili wa kipa huyo kuokoa mpira ya harari, Mrisho Ngasa aliipatia timu yake bao la pili baada ya

kuunasa mpira uliompita Job wakati akijaribu kuokoa na kuukwamisha langoni kwa shuti kali la juu. Lyon walibadilika na kuliandama lango la Simba na kufanikiwa kupata penati iliyopigwa na Shamte Ali na  kuokolewa na kipa wa Simba, Juma Kaseja. Hata hivyo Mwamuzi wa mchezo huo Israel Mujuni aliamru penati hiyo irudiwe kwa madai kuwa Kaseja alitoka langoni kabla ya mpira haujapigwa.

Pamoja na Shamte kupata nafasi hiyo, alipiga mpira nje na kuikosesha timu yake bao. Simba waliendelea kuliandama lango la Afrika Lyon. Ngasa aliipatia timu yake bao la tatu baada ya kupata pasi kutoka kwa beki wa kulia Nassoro Masoud, na kuwahandaa walinzi wa timu hiyo waliocheza bila mpangilio.

Kipindi cha pili Afrika Lyon walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Shamte Ali na Aman Kyata na kuwaingia Bright Ike na Hood Mayanja walioleta uhai kwa timu hiyom baada ya kuwapeleka puta Simba na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa Ike.

Makeke ya Simba yaliyonekana kipindi cha kwanza yalizimwa na vijana wa Lyon ambao waliliandama lango la Simba kama nyuki, lakini walishindwa kusawazisha magoli hayo kutokana na kila mmoja kuwa na tamaa ya kutaka kufunga.

Kipindi cha kwanza Kocha wa Simba Patrick Lewig alitoa mpya ya mwaka uwanjani, baada ya kuwaita wachezaji Mrisho Ngasa na Amri Kiemba kuwaonesha mnbinu za kuipenya ngome ya Lyon kwa Komputa ndogo. Kila mchezaji aliitwa kwa wakati wake wakati mchezo uliposimama kwa muda.

Simba iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nassoro Masoud, Paul Ngalema, Mussa Mude/ Kigi Makassi, Shomari Kapombe, Jonas Mkude/ Koman Keita, Mwinyi Kazimoto, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Ramadhan Chombo.

African Lyon; Abdul Seif, Fred Lewis, Jacob Massawe, Mohamed Samatta, Abdulghan Gulam, Yusuf Mpilipili, Jackson Kanywa, Aman Kyata, Ibrahim Issack, Shamte Ali na Juma Seif 'Kijiko'. 
 Kipa wa African Lyon Abdul Seif akijaribu kuokoa mpira miguuni mwa kiungo wa Simba Amri Kiemba
 Mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngassa (kulia), akijaribu kuwapita walinzi wa Afrcan Lyon
Ngassa akifunga bao la tatu Uwanja wa Taifa leo
 Ibrahimu Job wa African Lyon akijaribu kumlinda Ngassa asilete madhala kwenye lango lake.

 Amri Kiemba akichuana na Job wa Lyon (kushoto)
Mfungaji wa bao la Lyon Ike 28 akijaribu kumtoka Keita wa Simba





Kocha wa Simba akitoa maelekezo kwa Ngassa kupitia Komputa ndogo leo.


Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU