Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Cresentius  Magori (picha ya juu) na Mkuu wa Chapa ya Vodacom na Mawasiliano, Bw. Kelvin Twissa (chini), wakizungumza na waandishi wa habari, JB Belmont, Dar es Salaam leo, wakati wakizindua huduma mpya ya malipo ya michango kwa wanachama wa NSSF kwa njia rahisi ya M-PESA.

 Zaidi ya wanachama 6,000 wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanzia sasa hawana sababu ya kutembelea ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuwasilisha michango yao kutokana na kurahishwa kwa utaratibu wa uwasilishaji wa michango ambapo wanaweza kufanya hivyo kupitia simu zao za mikononi kwa njia ya M-pesa.

Utaratibu huo mpya ambao unawaunganisha wanachama wa NSSF na wateja zaidi ya 10 Milioni wa  kampuni ya simu ya Vodacom umezinduliwa rasmi Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Uendeshaji wa
NSSF, Bw. Cresentius Magari kwenye Hoteli ya JB Belmonte, akimwakilisha <kurugenzi Mkuu wa
shirika hilo, Dkt. Ramadhan Dau.

“Leo tunatangaza utaratibu mpya na rahisi ambao utawawawezesha wanachama wetu hususani walio
katika sekta isiyo rasmi kuwa na utaratibu rahisi kabisa katika historia ya uwasilishaji michango kwa NSSF kwa njia ya simu ya mkononi ikiwezeshwa na huduma ya M-pesa.” alisema Bw. Magori.

Hata hivyo Magori amesema kuwa utaratibu huo mpya wa uchangiaji kwa njia ya M-pesa hauzuii utaratibu wa zamani kwa wanachama wa mfuko huo kuwasilisha michango yao huku vikundi na taasisi kama TUJIJENGE, TAFF, AMSHA GROUP, THT na wanachama wengine kutoka vikundi vilivyojipanga chini ya mfumo wa uanachama wa hiari vikitazamiwa kunufaika zaidi na mfumo mpya wa M-pesa.

Kupitia uanachama wa hiari katika mfuko wa NSSF, kila mwanachama huchangia kuanzia Shilingi 20,000 kila mwezi. “Tunataka wanachama wetu hasa walio chini ya mfumo wa uanachama wa hiari ambao kimsingi
hawana mifuko rasmi ya akiba ya uzeeni na hivyo NSSF inawapatia nafasi ya kujiwekea akiba wawe na njia rahisi zaidi itakayowapunguzia gharama za uwasilishaji michango yao na hivyo kuendelea kuwekeza kwa siku za baadae.”Aliongeza Dk Dau

Aidha, Mkuu wa Chapa ya Vodacom na Mawasiliano Bw. Kelvin Twissa akizungumzia huduma hiyo amesema kasi ya ukuaji wa huduma ya M-pesa nchini inaendelea kuthibitisha uimara na kuaminika kwa huduma hiyo na wadau mbalimbali.

“Kila wakati tunaangalia ni kwa namna gani wateja wetu wanavyoweza kuitumia huduma hii kujirahisishia maisha, ahadi yetu kwa Watanzania ni kuendelea kuiwezesha huduma hii kuwa salama, ya uhakika na kuaminika wakati wote.” alisema Bw. Twissa

“Tumeshawezesha kuzileta takribani nyanja zote za huduma za biashara katika viganja vya wateja wetu kupitia huduma hii ya M-pesa tukiwaunganisha na makampuni zaidi ya 200. Kazi ya ubunifu bado inaendelea na wateja wetu watazidi kuona mengi zaidi katika M-pesa ambayo uwezekano wake haukuwa rahisi hata kufikirika hapo kabla.”

Huduma ya M-pesa kwa sasa ina mawakala zaidi ya 40,000 nchi nzima na hivyo kuifanya huduma hiyo kuwa karibu na Watanzania mijini na vijini na kuwawezesha kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi na uhakika wakati wowote mahali popote.

Ili mwanachama aweze kuwasilisha mchango wake wa NSSF kwa njia ya M-pesa anapaswa kufuata
utaratibu ufuatao katika simu yake ya Vodacom

Piga *150*00#
Chague nambari 4 (malipo)
Ingiza nambari ya biashara (770770)
Ingiza nambari ya kumbukumbu (ambayo ni nambari ya uanachama ya mwanachama)
Ingiza kiasi cha fedha

Kuhusu Vodacom Tanzania
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na  jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.   Vodacom Foundation  ina nguzo kuu tatu: Afya,  Elimu na Ustawi wa Jamii.

Hadi  sasa taasisi hiyo  imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha,  imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa  na kampuni mama ya Vodafone
.
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia  teknolojia ya kisasa  ya  mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki  hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na  asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd. Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa  Super Brand (Chapa Bora Zaidi)  kwa miaka  mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.

Kwa mawasiliano:
Matina G. Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited.
Mlimani City Jengo namba 1. Ghorofa ya kwanza.
Simu namba: 0754 710 099
 Magori (kushoto) na Twisa, wakishikana mikono baada ya kuwaeleza waandishi wa habari jinsi huduma hiyo itakavyowasaidia wanachama kutoa michango yao kwa wakati.
Magori (kulia) na Twisa wakijibu maswali ya waandishi wa habari leo.
 "Tumejipanga vizuri kuhakikisha kuboresha huduma ya M-PESA iliyoaminiwa na watanzania wengi", anasema Twisa (kulia)
"Huduma hii itawasaidia wanchama kupunguza gharama za safari wakati wa kupeleka michango", anasema Magori.

Hapa wakikabidhiana hati ya makubaliano ya mpango wa huduma ya M-PESA kwa malipo ya wanachama wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)


Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Bi. Eunice Chiume akizungumza na Bw. Twisa wa Vodacom, baada ya kuzindua huduma hiyo, kwenye Hoteli ya JB Belmont, Dar es Salaam leo

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU