YANGA YAIFANYIA KWELI AFRICAN LYON YAIKANDIKA 4-0

 Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kupenya katikati ya mstu wa walinzi wa African Lyon, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 4-0
Sunday Bakar wa Lyon akijaribu kumchunga Kiungo wa Yanga, Niyonzima asilete hatari langoni mwake.
Simon Msuva wa Yanga akipiga mpira kuelekea kwenye lango la Lyon, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo.
Washambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (katikati), Hamis Kiiza (kulia) na Simon Msuva wakishangilia bao la kwanza la Yanga dhidi ya African Lyon, lililofungwa na Tegete, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
 Hamis Kiiza wa Yanga (kulia), akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa African Lyon, Ibrahimu Job.
 Wachezaji wa Yanga Nadir Haroub Canavaro na Msuva wakishangilia pamoja na mfungaji wa bao la pili la Yanga lililofungwa na Jerry Tegete namba 10 leo.
Msuva akiwahamasisha mashabiki wa Yanga kushangilia
Mshambuliaji wa Yanga, Didie Kavumbagu akichuana na mabeki wa African Lyon, Yusuf Mlipili (kulia) na Sunday Bakari.
Picha ya juu na chini, Wachezaji wa African Lyon wakimzonga mwamuzi Martin Saaya wa Morogoro baada ya mchezaji mmoja wa timu hiyo kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na mwamuzi huyo kuamru ipigwe penati.

 Kiiza (kulia) na Ibrahim Job
 Said Bahanuzi akikata mbuga huku akilindwa vilivyo na mlinzi wa Lyon Aman Kyata.
 Kipa wa Lyon Abdul Seif akipata matibabu baada ya kuumia uwanjani leo
Kuingo wa Yanga Haruna Niyonzima akimlalamikiwa mshika kibendera Omar Kambagwa, baada ya kuonesha kibendera
Pongeni kwa Tegete aliyefunga bao la pili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU