MINZIRO NGUZO YA UHAKIKA YANGA

MSHAMBULIAJI wa Yanga Didier Kavumbagu (pichani), amesema,aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga Fred Felix Miziro alikuwa muhimili katika mazoezi ya Klabu hiyo zaidi ya Kocha Brandts aliyetimuliwa.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa haelewani na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Ernie Brandts kutokana na kila mara kumuweka benchi huku akijitahidi kujituma mazoezini.

Bifu la Kavumbagu na Brandts lilianza katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Oljoro ambapo mchezaji huyo aliwekwa benchi na kukataa na kuamua kuvaa nguo za nyumbani.

Hali hiyo imepelekea kocha huyo kutimuliwa baada ya mechi ya Mtani Jembe Yanga ilipokubali kipigo cha mabao 3-1,kutokana na timu kuonekana kucheza katika kiwango cha chini.

Mbali na hilo Brandts alionekana kushindwa kuzibiti nidhamu za wachezaji kutokana na baadhi yao kufanya mambo wanayotaka.

Mbali na Brandts,uongozi wa Yanga umeamua kuwaondoa kocha msaidizi Fredy Flex Minziro,kocha wa makipa Razaki Siwa na Daktari wa timu hiyo Nasoro Matuzya.

Akizungumza na Spoti Starehe mara baada ya kumaliza mazoezi katika uwanja wa Bora Kijitonyama Kavumbagu alisema,anayakubali zaidi mazoezi ya Minziro kwani yanampa muda wa kupunzika.

"Kwangu mimi mazoezi anayotupa kocha Minziro mazuri zaidi kulinganisha na Brandts kwani yananipa muda wa kupunzika jambo ambalo kwa mchezaji yoyote lazima ayafuraie",alisema.

Aliongeza kwa kusema,sio kama mazoezi waliokuwa wakipewa na aliyekuwa kocha wao Brandts yalikuwa hayafai ila kocha Minzio yapo mazuri zaidi.

Kavumbagu raia wa Burundi ambaye alisajiliwa na Yanga akitokea Atletical msimu uliopita ambaye mpaka sasa katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara ameshatikisa nyavu mara tano.
 Aliposajiliwa kucheza Yanga
Akishangilia baada ya kufunga bao Uwanja wa Taifa.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU