NIYONZIMA KUONDOKA YANGA?

 KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (pichani), amesema, anaangalia maslahi iwapo kuna timu itamuhitaji yupo tayari kuondoka kwenye klabu yake ya sasa.

Mchezaji huyo raia wa Rwanda aliyesajiliwa Yanga akitokea APR mwaka 2011 amekuwa nguzo kubwa kwa timu ya Yanga kutokana na uwezo aliokuwa nao kwa kuisaidia timu hiyo msimu uliopita na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara na kuendelea kusimama kileleni mwa Ligi Kuu.

Niyonzima amekuwa akiwindwa na timu nyingi kutokana na umahili wake wa kusakata kabumbu lakini amekuwa akiheshimu mkataba wake na klabu ya Yanga.

Hata hivyo mchezaji huyo amesema,Yanga sio mwisho wake anachoangalia maslahi iwapo kama kuna timu inamuhitaji na wameafikiana vizuri hana budi kuondoka.

Spoti Starehe lilizungumza na mchezaji huyo juzi mara baada ya kumaliza mazoezi katika uwanja wa Bora Kijitonyama alisema,yupo tayari kuondoka kama itatokea timu yenye maslahi mazuri.

"Yanga sio mwisho wangu mi nachojari maslahi ukizingatia mpira ndio kazi yangu kwa hiyo kama timu hipo yenye mpunga mnene naondoka",alisema.

Aliongeza kwa kusema,zipo timu nyingi zimeshamfuata lakini amekataa kuzitaja ambazo zilikua azijafika katika maslahi yake mazuri.

Akimzngumzia aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Muhalanzi Ernie Brandts alisema,wamepoteza kocha mzuri itachukua muda timu kukaa sawa.

Alisema,timu ilikuwa ikielewana kwa kiwango cha hali ya juu mpaka ikafanikiwa kuwa bingwa na mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara msimu huu imekuwa ya kwanza.

Hata hivyo alisema,watajitahidi kujituma kadri ya uwezo wao na kumpa ushirikiano kocha atakayekuja ingawa mfumo utabadirika.

Alisema,mpaka sasa hawajui hatma ya timu yao kwani hata kombe la Mpinduzi wameshindwa kwenda ambalo lingekuwa kipimo tosha cha kujipima kuelekea kwenye igi kuu mzunguko wa pili.
Hapa Niyonzima akifanya vitu vyake Uwanjani.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU