TUMEWASIKIA WASOMAJI WETU, TUTARUDIA HADITHI YA NJAMA

Wapendwa wasomaji wa Blog ya MPIGANAJI. Nyakasagani.blogspoti.com, tunapenda kuwaomba radhi kutokana na usumbufu wa kukosa hadithi ya kusisimua ya NJAMA iliyokuwa ikitoka kupitia Blog hii. Ukweli ni kwamba tuliendelea na hadithi hii hadi mwisho, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo baadhi ya wasomaji wetu hawakuendelea na hadithi hii ya upelelezi inayosisimua sana.

Sisi MPIGANAJI, tunaamini kuwa wasomaji wetu wana shauku kubwa ya kujua hatm,a ya silaha za wapigania uhuru wa Afrika Kusini zilizoibiwa Bandarini, Jijini Dar es Salaam, kutokana na baadhi ya mataifa kuinyooshea kidole serikali ya Tanzania huku mataifa mengine yakisema kuwa Tanzania haiwezi kuhusika na wizi wa silaha hizo kutokana na jitihada zake za kuikomboa Afrika kutoka mikononi mwa Makaburu.

Kutokana na maombi ya wasomaji wetu, ambao ndio wadau wakubwa wa Blog hii, tumeshawishika kurudia hadithi hii, kuanzia sehemu ya Binti Tanzania, ambayo wasomaji wetu waliotupigia simu hawakubahatika kuipataa. Kutokana na hali hiyo. Tunalazimika kusimamisha kwa muda hadithi ya OFU inayoendelea. hadithi hiyo pia inahusu upelelezi ukombozi Kusini mwa Afrika.

NYAKASAGANI MASENZA,
MRATIBU MKUU
MPIGANAJI BLOGSPOTI

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru