SIKUJUA
Wazazi wake walikuwa wamekata tamaa ya kupata mtoto wakati
mimba ilipotungwa bila wao kutarajia. Jitihada za wataalam wa kisasa na wale wa
asili zilikuwa zimegonga mwamba.
Kila mmoja alistaajabishwa na ujauzito ule wa ghafla!!
Akazaliwa mtoto wa kike wakamuita SIKUJUA….
Na kweli hawakujua na hakuna aliyejua!!
Mzee Chapakazi haupati wasaa wa kuishi muda mrefu na binti
yake wa pekee, katika namna ya ghafla sana anaugua na kuaga dunia! Anamuachia
maagizo mazito mkewe juu ya binti yao Sikujua.
Mama Sikujua anayapokea na kuyahifadhi moyoni.
Sikujua akakua kwa hekima na kimo, akautambua ugumu wa maisha
na kujidhatiti katika elimu, Akavuka madarasa na hatimaye vidato….
Alijifunza mengi katika elimu ya darasani lakini hakuikumbuka
elimu dunia!!
Hatimaye akakutana na upepo wa mapenzi ukaanza kumpeperusha na
hatimaye akajikuta anafanya jambo zito bila kujua madhara yake!!
Baada ya miaka kadhaa akiwa anafurahia maisha zimwi lile
alilodhani amelizika miaka kadhaa nyuma likamrudia!! Tafsiri ya jina lake ikaja katika uhalisia lakini tayari
alikuwa amechelewa sana………
Ni jambo gani lililomtafuna Sikujua na nini hatma yake!
Fungua ndani uburudike na kujifunza kutoka katika mkasa huu
ulioegemea katika maisha halisi….
NI HADITHI MPYA KUTOKA KWA MTUNZI MAHIRI ANAYEFAHAMIKA KAMA
‘CHANGAS MWANGALELA’ KITABU HIKI SI CHA KUKOSA, KWANI KINA MENGI YA KUJIFUNZA
KATIKA MAISHA TUNAYOYAISHI MIMI NA WEWE.
KIMEINGIA SOKONI JUMATATU MARCH 17, 2014.
JIPATIE NAKALA YAKO KWA BEI POWA KABISA YA Tsh 7000/=
KWA MAWASILIANO PIGA
NAMBA 0713 193 002 & 0753 172654, ILI UJIPATIE NAKALA YAKO!!!!
Comments
Post a Comment