Analog Clock

NSSF

NSSF
NSSF TANGAZO

Tone Radio Tz

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Monday, May 12, 2014

WARIOBA, MWANAFUNZI MWENYE KIPAJI CHA KUCHORA PICHA HALISI

WARIOBA NYAKASAGANI (PICHANI), NI MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO KATIKA SHULE YA MSINGI HIGHMOUNT, ILIYOKO GONGO LA MBOTO, MANISPAA YA ILALA, DAR ES SALAAM, AMBAYE SIFA NA KIPAJI CHAKE CHA KUCHORA PICHA HALISI KINAWAVUTIA WANAFUNZI WENZAKE AMBAO WANAMWITA JAJI WARIOBA NOMA.

KIPAJI CHA WARIOBA KILIANZA KUONEKANA AKIWA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI MUUNGANO ILIYOKO CHANG'OMBE, MANISPAA YA TEMEKE, AMBAKO ALIWEZA KUCHORA PICHA HALISI ZA WATU MBALI MBALI WAKIWEMO WALIMU NA WANAFUNZI WENZAKE.

HIVI KARIBUNI WARIOBA ALITIA FORA BAADA YA KUCHORA PICHA HALISI YA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALASIA ILIYOPOTEA, AKITUMIA PICHA ZILIZOSAMBAA KWENYE MAGAZETI. HII INAONYESHA KUWA MTOTO HUYU ATAKUWA MCHORAJI MZURI SIKU ZA USONI, TUMSAIDIE ILI KIPAJI CHAKE KISIPOTEE.

No comments:

Post a Comment