HOFU

ARUSHA

VIII

Ilikuwa saa nane za mchana wakati F.K aliporudi. Alikuta wenzake wamelala. Walihitaji usingizi kwani usiku huo walitarajia kuwa macho. Alienda moja kwa moja kwenye chumba ambamo Peter Gerrit, George na Dave walikuwa wamepumzika.

"Karibu, F.K", George alimkaribisha. Yeye tu ndiye aliyekuwa hajalala. "Una mapya yapi?".

"Ninayo mengi", F.K alijibu. Wakati huo huo Peter na Dave wakazinduka kutoka usingizini.

"Kwanza Tondo nimemkuta ofisini?", F.K aliuliza. "Anasema kuwa Hamisi alimpigia simu na kumweleza kuwa Willy alimshauri aweke vijana wa usalama kumfuatilia na kuripoti mienendo yake yote. Hivyo nimemshauri akitoka ofisini aende moja kwa moja nyumbani kwake na asitoke".

Aliposikua hivyo George aliinuka kitandani.

"Hapana F.K", George alisema na kuinuka kitandani. "Tondo lazima auawe"."Auawe? Hapana, mtu huyu ametusaidia sana", F.K alimtetea Tondo. "Lazima aishi ili naye aweze kufurahia ushindi. Bila yeye mimi nisingeweza kufanya yote niliyofanya hapa nchini. Taarifa zote za kijasusi nilizoleta ni kutokana na msaada wake, kwani yeye alikuwa afisa wa cheo cha juu katika jeshi la polisi. Hapana, George, Chris Tondo lazima aishi ili afaidi matunda ya ushindi wetu. Vile vile nimeamua kwenda naye Afrika Kusini baada ya kazi ya hapa".

Wale majasusi wengine walimwangalia kwa macho makali yenye kutoa onyo.

"Nafikiri litakuwa jambo la busara kwako kufanya hivyo", P.G. alimwasa F.K.

ITAENDELEA

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru