HOFU

ARUSHA

X

Wakati wenzake walipokuwa wamepumzika, mnamo saa kumi za mchana, Willy alimpigia simu ndugu Mbeki. Mbeki alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kutayarisha mkutano. Alikuwa amefikia Maunt Meru Hoteli.

"Hallo. Maunt Meru hapa", mpokeaji simu alisikika akisema.

"Nipe chumba 321", Willy alisema.

"Subiri".

"Hallo, Mbeki hapa".

"Aha, nimepata habari kuwa unanitafuta".

"Sawasawa, naomba uje tuonane hapo kwenye klabu ya Kituo cha mikutano ya Kimataifa. Unaifahamu?", Willy aliuliza.

"Basi, jitahidi uwe pale katika muda wa dakika kumi zijazo".

"Haya".

Willy aliweka simu chini na kutelemka chini.

Alichukua teksi na kuelekea AICC Klabu.

Alipofika alisubiri kidogo na Mbeki akawasili. Willy alikuwa anajulikana sana mahali hapo. Aliongozana na Mbeki mpaka kwenye kibanda kimoja, halafu wakaagiza vinywaji.

"TUmekuwa na wasiwasi sana baada ya matukio makubwa ya jana", Mbeki alianza.

"Hiyo ndiyo sababu imetuleta hapa", Willy alijibu.

"Ulinzi wa Polisi unaonekana ni dhaifu sana", Mbeki alisema. "Viongozi wote wanawasili leo jioni, tayari kwa mkutano wa kesho. Sasa mimi ninao wasiwasi. Kuna mtu ambaye anatoa habari zetu nje, lakini hatujui ni nani".

"Mimi nashauri kuanzia sasa mtoe habari kwa mtu yeyote. Ikibidi punguzeni watu hata kwenye kamati ya matayarisho. Bakizeni watu tunaowafahamu fika. Sasa nisikilize kwa makini. Nataka ufanye kama nitakavyokueleza. Usikose hata chembe, kwani ukikosea, kutatokea balaa isiyoelezeka", Willy alitahadharisha.

Alianza kumweleza Mbeki juu ya mipango yote ya usalama wa mkutano kuanzia dakika ile mpaka mwisho wa mkutano. Alimweleza mipango ya ulinzi wa wajumbe, na viongozi mashuhuri wa wapigania uhuru.

ITAENDELEA

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru