Analog Clock

NSSF

NSSF
NSSF TANGAZO

Tone Radio Tz

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Sunday, June 8, 2014

MTEMVU AWAAPISHA MAKAMANDA WA VIJANA WA CCM KATA 14

Mbunge wa Temeke (CCM), Bw. Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na wana CCM wa Kata 14, Temeke Dar es Salaam, baada ya kuwaapisha Makamanda wanne wa matawi ya chama hicho. Wa pili kushoto ni Bw. Gogo Mzome Tawi la Temeke, Bw. Omari Shomvi tawi la Matumbi, Bi. Amina Mlewa tawi la Njaro na Bw. Umaru Habibu wa tawi la Maganga. Kushoto ni Kamanda wa Vijana wa Kata hiyo Bw. Iddy Ngozi.

Mbunge wa Temeke (CCM), Bw. Abbas Mtemvu (kulia) akimvisha joho la Ukamanda wa vijana wa CCM, Kamanda wa Vijana Tawi la Njaro, Bi. Amina Mlewa, baada ya kuwaapisha makamanda wanne wa matawi ya chama hicho Kata 14, Temeke, Dar es Salaam
Wakeleketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Matumbi, wakiwa wamembema Kamanda wao wa Vijana wa CCM wa tawi hilo, wakimsindikiza kwenda kuapishwa rasmi kuwa Kamanda wa Vijana wa Tawi hilo, kazi iliyofanywa na Mbunge wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu, Temeke, Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Temeke (CCM), Bw. Abbas Mtemvu (kulia) akimvisha joho la Ukamanda, Kamanda wa Vijana wa CCM Tawi la Temeke, Bw. Gogo Mzome, baada ya kumuaapisha yeye na makamanda wenzake wanne wa matawi ya chama hicho Temeke, Dar es Salaam


Mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata 14, iliyoko Temeke, Dar es Salaam (katika picha juu na chini), wakiselebuka kwa kucheza na kushangilia kwa furaha baada ya Mbunge wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu, kuwaapisha Makamanda wanne wa vijana wa matawi ya Njaro, Matumbi, Temeke na Maganga.

No comments:

Post a Comment