TANZANIA YAFANYA KWELI KWA ZIMBABWE, YAWASUBIRI MAMBAZ WA MSUMBIJI

KIKOSI CHA TANZANIA 'TAIFA STARS', KILICHOSONGA MBELE BAADA YA KUPATA SARE YA 2-2 KATIKA MJI WA HARARE, ZIMBABWE JANA KUWANIA TIKETI YA KUCHEZA FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA NCHINI MOROCCO MWAKANI.
ZIMBABWE WALIHITAJI USHINDI WA 2-0 DHIDI YA STARS ILI WASONGE MBELE LAKINI..
MUUAJI WA ZIMBABWE, THOMAS ULIMWENGU ANAYEKIPIGA KATIKA KIKOSICHA T.P MAZEMBE YA KONGO, AKIONESHA UWEZO WAKE UWANJANI DHIDI YA ZIMBABWE
THOMAS ULIMWENGU (KUSHOTO), AKIWAJIBIKA UWANJANI

NYAKASAGANI MASENZA\

TANZANIA imetinga katika hatua ya pili ya michuano ya Afrika, kuwania kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika nchini Morocco mwaka 2014, baada ya jana kuwafungashia virago jirani zao Zimbabwe, katika mchezo mkali wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Mjini Harare, Zimbabwe.

Mchezo huo uliokuwa mkali wa kusisimua, wenyeji walianza kupata bao dakika ya nne, lakini Watanzania kupitia kwa Nahodha wake Nadir Haroub 'Canavaro', walisawazisha dakika ya 21. 

Kipindi cha pili Watanzania walirejea uwanjani kwa matumaini ya kusaka ushindi, ambapoThomas Ulimwengu aliyekuwa mwiba katika safu ya ushambuliaji ya Stars aliwapatia Watanzania bao la pili lililosawazishwa na wenyeji na kusababisha matokeo kuwa 2-2 na Tanzania kusonga mbele ikiwasubiri Msumbiji, ambao watakutaka katika mchezo wa kuwania tiketi hiyo mhimu.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU