Analog Clock

NSSF

NSSF
NSSF TANGAZO

Tone Radio Tz

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Saturday, September 27, 2014

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WATEMBELEA MIRADI YA NSSF

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akijibu maswali ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, walipotembelea mradi mkubwa wa uwekezaji katika Kijiji cha DEGE Eco, Kigamboni, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Lodovick Mroso na Meneja Kiongozi wa Mahusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume.
 
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (kulia), akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wanaotembelea mradi mbalimbali ya uwekezaji unaofanywa na NSSF. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Creasentius Magori.

Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakijaribu kupita kwenye njia ya dharura, kwa ajili ya kupanda juu kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka, wakati akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri hao, walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa
Wahariri wa Vyombo vya Habari wakimshuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akipita kwenye kwenye kivuko cha muda, wakati wakitoka kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana.Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka, wakati akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF.


Wahariri wa Vyombo vya Habari wakipita kwenye daraja la muda, lililojengwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi, walipofanya ziara ya kuangalia miradi mikubwa ya uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment