WAJUMBE HALMASHAURI KUU YA CCM WAKAGUA UJENZI WA DARAJA KIGAMBONI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pili kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa tatu kushoto), wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ramadhani Madabida  (wa tatu kulia), akimsikiliza Mhandisi Karrim Mataka wa NSSF (wa pili kulia), wakati Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipotembelea mradi wa daraja la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pilia kulia) aliyefuatana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walifika kukagua maendeleo ya mradi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, Bw. Ramadhani Madabida.

"Kama mnavyoona kazi inaendelea kwa kasi, Daraja linakuwa tayari mapema iwezekanavyo", Mhandisi Karrim Mataka akiwaeleza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.
Wakipita kwenye daraja la muda, lililoandaliwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi wa daraja hilo.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU