TRAFIKI WA KUJITOLEA DAR ES SALAAM

Katika jitihada za kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Mlinzi huyu wa Makampuni binafsi amekutwa akisaidia kuongoza magari kwa ustadi mkubwa, katika Barabara ya Zanaki leo

Akiwa ameyazuia magari kutoka upande mmoja wa Barabara ili kuruhusu magari ya upande mwingine yapiteAkionyesha ishara kwa madereva wanaokwenda kulia kufanya hivyo ama wanaokwenda moja kwa moja

Akiangalia kama kuna magari mengine kutoka upande wa pili kabla ya kuruhusu magari yapite. Akizungumza na dereva aliyeonekana kukaidi amri yake. Hata hivyo Dereva huyo alitii amri na kusimama.Akifanya manjonjo kama wafanyavyo Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wanapoongoza magari. Hapati ujira, halipwi chochote, lakini ameguswa kusaidia kupunguza msongamano wa magari, tusimbeze.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru