WATANO WANUFAIKA NA BAHATI NASIBU YA BENKI YA AFRIKA

Meneja Biashara wa Benki ya Afrika (BOA TANZANIA), Bw. Solomon Haule (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kabla ya Mchezo wa Bahati Nasibu kwa wateja wa benki hiyo, uliochezeshwa Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Mawasiliano BOA, Bw. Willington Munyanga na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid (kulia).
Na Nyakasagani Masenza, Dar es Salaam

Washindi watano wa Bahati Nasibu ya Benki Afrika wametangazwa leo, ambapo Mshindi wa kwanza, Bw. Edmund Michael Assenga, Mshindi wa pili Bw. Gichan Athuman Iddi, Mshindi wa tatu, Bw. Yong Wang Li, Mshindi wa nne, Bw. Sajid Abdulrahman Halidy na Mshindi wa tano ni, Bw. Leakev Tom Gathuri.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Meneja Biashara wa Benki ya hiyo, Bw. Solomon Haule amesema, ili kurejesha faida ya benki kwa wanachama, wameamua kutoa motisha kwa kuchezesha mchezo wa kubahatisha ambapo mshindi wa jumla atashinda gari mpya aina ya TOYOTA Saloon.

Bw. Haule amewaasa watanzania na wananchi kutoka mataifa mbalimbali duniani, wanaoishi nchini kutunza fedha zao BOA kwani ndio benki inayotoa faida kubwa kwa jamii. "Leo tumetoa washindi watano, shindano hili ni endelevu, mpaka tutakapofikia tamati, ambapo mshindi wa jumla atapatikana na kushinda gari mpya kabisa kutoka Toyota", amesema Bw. Haule Dar es Salaam leo.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru