YANGA KULIPA KISASI KWA MGAMBO JKT LEO


KIKOSI CHA YANGA 

LIGI Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo, katika mzunguko wa saba, huku Vijana wa Jangwani chini ya Kocha, Marcio Maximo Yanga wakipania kulipa kisasi kwa Mgambo JKT ya Handeni Tanga, iliyotia ndimu safari ya Yanga kutwaa Ubingwa msimu uliopita.

Mchezo wa leo unatalajiwa kuwa mkali nawenye ushindani wa aina yake hasa baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 mwaka jana na kupoteza mchezo wa raundi ya sita dhidi ya Kagera Sukari, uliochezwa mkoani Kagera, nao Mgambo wakipata sare dhidi ya Mbeya City mkoani Tanga.

Katika mchezo wa leo, Kikosi cha Yanga kitawakosa wachezaji wake nyota, Nahodha Nadir Haroub Canavaro aliyepewa kadi nyekundu mkoani Kagera wakati Yanga ikilala bao 1-0 na mlinzi kisiki Kelvin Yondan mwenye kadi tatu za njano, ambazo zinamfanya asicheze mchezo wa leo.

Kutokana na pengo hilo, Yanga italazimika kuwatumia wachezaji wake kama Zahir na Salim Telela, ambao wamekuwa benchi kwa muda mrefu, katika safu ya ushambuliaji timu inatarajiwa kuwapa nafasi akina Jerrison Tegete na Husein Javu walioonyesha uhai wakati wa mchezo dhidi ya Stand United.

Mbali na mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam majira ya saa kumi alasiri. Mabingwa watetezi Azam watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Chamazi kuwakaribisha ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union kutoka Tanga, Mtibwa Sukari watawakaribisha ndugu zao Kagera Sukari, Stand United na Mbeya City.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru