KWA UPUUZI WA MAXIMO NI NDOTO YANGA KUWASHINDA SIMBA

 Kocha Mkuu wa Yanga Marcio Maximo, ambaye uongozi na mashabiki wa Yanga wamemchoka
 Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Canavaro', alifanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi.
 Kpah Sherman alionyesha uwezo mkubwa japo hakupata msaada
Emerson Oliveira, alionyesha kiwango kidogo wakati Yanga ilipocheza na Simba
 Winga Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva ambaye uwezo wake haulingani na wachezaji wa MaximoKikosi cha Yanga kilicholambishwa subiri na Simba, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

“Ni ndoto ya mchana Yanga kuwafunga mahasimu wao Simba”, Ndivyo unaweza kusema, itabaki kuwa historia kwani wapinzani wao wanajuwa mbinu za kuwafunga, wakati ushindi wa Yanga ni sare. Kasumba iliyojengwa na viongozi wa Yanga kukimbilia kusajili kila mchezaji anayetakiwa na Simba itaendelea kuwafanya wafungwe kila watakapokutana, hali hiyo ikichagizwa pia na Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Mbrazil, Marcio Maxime.

Hivi karibuni Simba ilitangaza kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Polisi Morogoro, Danny Mrwanda, baada ya Yanga kupata tetesi, viongozi wa Klabi hiyo walifanya mipango ya haraka kumsajili kana kwamba wanawakomoa Simba, kumbe wanaongeza mamluki ndani ya klabu.

Hakuna asiyefahamu kuwa Mrwada ni mchezaji na mwanachama hai wa Simba, na uongozi wa Simba kutaka kumsajili ni mkakati mojawapo wa kumrejesha kundini kada huyo aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

Waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako, kwa kiasi Fulani Simba imewekeza wachezaji wao ndani ya Yanga, wakati Yanga wenyewe hawajawekeza ndani ya Simba,  kwa hali hiyo, Yanga isitegemee miujiza kuwafunga Simba.

Mtoto wa nyoka ni nyoka, Ndani ya Yanga wapo nyoka kama, makipa Ali Mstafa, Deogratius Munis na Juma Kaseja (anayeondolewa msimu huu, mlinzi kisiki Kelvin Yondan aliyesajiliwa Yanga mwaka jana na sasa wamemchukua kada mwingine mwandamizi wa klabu hiyo ya Msimbazi Danny Mrwanda na Amis Tambwe ambaye Simba wameona kiwango chake kimeshuka. 

Kuhusu Kocha Maximo, ataendelea kuwaudhi mashabiki wa Yanga kwa kuwaleta wachezaji wenye uwezo mdogo ili wachezaji wenye wazawa wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka wasipate namba. Kitendo cha Maximo kuwaleta ndugu zake Emerson Oliveira na Andrey Coutinho na kuwaacha Jerryson Tegete, Hussein Javu, Nizar Khalfan na Salim Telela wenye uwezo mkubwa ni kuiangamiza Yanga.

Wakati umefika Yanga watambue kuwa si kila Kocha kutoka Brazil ana uwezo, hebu tuwapatie kazi makoche wetu wazalendo, wenye mapenzi makubwa na Yanga kama Boniface Mkwasa, Fred Minziro na Juma Pondamali. Hakika Yanga itafanya vizuri, poleni wana Yanga wote.  

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru