KWAHERI MAXIMO, HUKUWA NA JIPYA YANGAMCHEZO wa Nani Mtani Jembe, unaozikutanisha timu mbili kongwe zenye upinzani wa jadi nchini, Yanga na Simba imegeuka kuwa machinjio kwa makocha wa Yanga baada ya Kocha Mkuu wake Mbrazil Marcio Maximo kutimuliwa rasmi jana kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba. 
Huu ni msimu wa pili mfululizo, kwa Yanga kuwafukuza makocha wake baada ya kufungwa na Simba, kwa kupoteza mchezo wa nani mtani jembe. Mchezo wa kwanza uliofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi.

 MARCIO MAXIMO

Mwaka huu Kocha Marcio Maximo nae amefungashiwa virago baada ya timu yake kungwa mabao 2-0 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Maximo aliyepokelewa Jangwani na mashabiki wa Yanga kwa vifijo na nderemo Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa Kocha mpya wa timu hiyo, amewaaga rasmi wachezaji wake wakati wa mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola Dar es Salaam jana.

Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwatakia maisha mema ndani ya Klabu hiyo ya Jangwani huku akionekana mwenye shauku ya kutaka kuendelea na kibarua chake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa kumuacha kocha wao akiwemo mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda. Mmoja wa wachezaji ambaye hakupenda kutajwa jina alisema "Ni kweli kocha ametuaga, lakini angepewa muda!

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru