UTABIRI WA SHEIKH SHARIFF WAZUSHA GUMZO NCHINI

MTABIRI WA NYOTA SHEIKH SHARIFF MATONGO AKIONGEA NA WAANDISHI LEO

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mtabiri wa nyota Sheikh Shariff Matongo amezungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, akidai kuwa ameoteshwa ndoto na Mwenyezi Mungu na kupata ushauri kutoka kwa Masheikh mbalimbali Duniani kuwa  mambo mazito saba yatatokea likiwemo la mchakato wa kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015, ambaye nyota zinaonesha nafasi hiyo itashikwa na mtanzania aliyeishi nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

Sheikh Shariff amewaambia waandishi wa habari kuwa,mwaka 2015 kitatokea kifo cha kiongozi mzito, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama tawala (CCM). Amesema pia zitanyesha mvua nyingi na watu waishio mabondeni watasombwa na mafuriko, vitatokea vifo vingi vya watoto, baadhi ya wafanyabiashara watapata mafanikio mwaka 2015.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa, nyota zinaonyesha vijana wengi watang'ara na kushinda Ubunge na Udiwani katika uchaguzi mkuu ujao. Amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nyadhifa hizo kwani wazee wengi watapoteza nafasi hizo.

"Baada ya kuota ndoto hii sikukaa kimya, niliuliza na kutafuta ushauri
kwa watu mbalimbali duniani, mfano nimeongea na Mufti wa Abhudhabi,
Nigeria na wengine ambao wamenishauri nisikae kimya, ndio maana
nikawaita kuwafahamisha kuhusu utabiri wangu", amesema Sheikh Shariff
Matongo.

Kuhusu usafiri na majini, Sheikh Shariff amesema utakuwa na misukosuko
ya hapa na pale kwani bahari itachafuka na kusababisha mawimbi mazito na
hatimaye chombo kimoja kitazama kutokana na hali hiyo amewataka watoa
huduma ya usafiri wa majini kuwa makini.

Sheikh Shariff amewaasa watanzania kuzingatia maoni na ushauri wake
kutokana na ndoto hizo. Hata hivyo alipoulizwa kama amewahi kuota ndoto
zenye mtazamo kama hiyo hakuwa tayari kutoa maelezo isipokuwa
amesisitiza kuwa ndoto yake isipuuzwe.

Kazi kwenu mnaotafuta Unyerere wa Tanzania kwa udi na uvumba, mtabiri
anasema nyota inaonyesha mrithi wa Rais Kikwete lazima awe ameishi nje
ya Tanzania kwa muda mrefu. Huyo hatufai, kama anaishi nje ya Tanzania
kwa muda mrefu hatakuwa chaguo halisi la watanzania.

Watanzania wanahitaji kiongozi wanayemfahamu, awe karibu na wananchi kwa shida na raha, awe ameishi ndani ya Tanzania akiyajuwa vizuri matatizo
ya watanzania, mtu aliyeishi nje ya Tanzania kwa muda mrefu ni dhahili
kuwa haujuwi vizuri utanzania wake, yawezekana akaja na heleni masikioni
ama kidali mguuni, huyo atakuja kwa ajili ya kuuza nchi.

Ni jambo lisilotia shaka kuwa watanzania wanasubiri kwa shauku kubwa
kipyenga cha mbio za urais, Ubunge na udiwani ili wawachague viongozi
wawapendao. Watanzania wengi wametangaza nia ya kugombea urais. Kila
mmoja akiwa na siri yake moyoni.

Watanzania waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo hadi sasa ni Wawaziri
Mkuu Mizengo Pinda, ambaye hata hivyo anatajwa kuwa hana sifa kutokana
na kushindwa kuonyesha uwezo kwenye nafasi aliyonayo sasa. Wengine ni
Mawaziri Wakuu Wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, Mawaziri
Benard Membe wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Lazaro
Nyarando wa Maliasili na Utalii, Mark Mwandosya asiye na Wizara maalum
na Steven Wassira wa UMahusiano na Uratibu Ikulu.

Wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Mwana mama pekee Asharose Migiro.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru