UCHU

 NGUVU YA RUSWA

II

Willy Gamba akifuatana na Bibiane usiku huo, huku mkononi mwake ameshika bunduki kubwa aina ya AK 47, walitembea kwa tahadhari kubwa kuelekea nyumbani kwa Col. Rwivanga. Walipofika hawakumkuta na nyumba yake ikiwa imefungwa. Kwa vile Willy alikuwa amepewa ufunguo wa ziada, walikuwa wameamua kwa ajili ya swala la kiusalama Willy awe analala pale, Alifungua mlango na kumvuta Bibiane ndani. Aliwasha taa ya sebuleni na kumsukumia Bibiane kwenye kochi.

Kwa mara ya kwanza ndipo Willy alipomwangalia Bibiane vizuri. Alistaajabu kuona kiumbe kizuri kama hiki kilivyojiingiza kwenye vitendo vya ugaidi wa ajabu. Hakika huyu msichana alikuwa mzuri. Ukisikia mrembo, urembo hio huu. Willy katika maisha yake alishawaona wasichana warembo lakini huyu alikuwa msichana mrembo kwelikweli.

"Asante kwa kuniokoa", Bibiane alimshukuru Willy Gamba huku akiwa amelegeza macho yake na kuonyesha tabasamu la aina yake mbele ya Willy ambaye alikaa kimya akimwangalia bila kujibu.

"Sasa niko upande wako, usipate taabu kunilinda, kwa jinsi ulivyookoa maisha yangu sasa nifanye vyovyote upendavyo", Willy kwa kumwangalia Bibiane machoni aliamini kuwa anasema ukweli.

"Nenda kaoge", Willy alimweleza Bibiane huku akielekea kwenye chumba alichokuwa akilala. Bibiane aliinuka taratibu na kumfuata Willy. Chumba alichokuwa akilala kilikuwa na maliwato ya ndani. Hivyo, alimuonyesha ishara Bibiane alifungua mlango na kuingia ndani.


Wakati Bibiane anaoga, Willy aliingia jikoni na kutayarisha kahawa. Alipoangalia saa yake ilikuwa yapata usiku wa manane. Alishangaa kwa nini Col. Rwivanga alikuwa hajarejea,  akajiuliza ameelekea wapi wakati huo.

ITAENDELEA 0784296253

Comments

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru