BIBI AWASHANGAA MALAWI KUDAI SEHEMU YA ZIWA NYASA

BIBI MATHA NCHIMBI (96), MKAZI WA MBAMBA-BAY, WILAYA YA NYASA, MKOANI RUVUMA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NYUMBANI KWAKE, WAKATI AKIELEZEA MPAKA HALISI WA TANZANIA NA NCHI YA MALAWI. BIBI MATHA ALIYEZALIWA MBAMBA-BAY ANASEMA MPAKA HALISI WA NCHI HIZI UKO KATIKATI YA ZIWA NYASA.HII NI SEHEMU YA ZIWA NYASA, UPANDE WA TANZANIA BARA, ENEO AMBALO SERIKALI YA MALAWI INADAI NI SEHEMU YA NCHI HIYO. HATA HIVYO WAZEE WALIOZALIWA KANDO YA ZIWA NYASA WAMEISHANGAA MALAWI NA KUWA HUO NI UCHOKOZI KWA SERIKALI YA TANZANIA.HAPA NI UKINGONI MWA ZIWA NYASA KAMA INAVYOONEKANA KATIKA PICHA HII, MWALIMU NYERERE ALIWAHI KUFIKA ENEO HILI NA KUTOA TAMKO KUWA IWAPO MALAWI WANATAKA SEHEMU HII WAKUBALI KUILIPA TANZANIA SHILINGI MIA MOJA KWA KILA WIMBI LA MAJI LITAKAPOGONGA UKINGONI. MALAWI WAKASHINDWA.
BIBI MATHA NCHIMBI (KULIA), AMBAYE ALIZALIWA KARIBU KABISA NA UKINGO WA ZIWA NYASA MIAKA 96 ILIYOPITA, AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI  MWANDAMIZI WA  ZBC, MSHANGU SAID, ALIPOMTEMBELEA NYUMBANI KWEKE MBAMBA-BAY, NYASA.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru