Meneja
Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu droo
ya mwisho ya Pormosheni ya ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.
Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel Moya na Afisa
kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.
.................................................................................................................................
DAR ES SALAAM LEO
Mteja wa
Benki ya Afrika Tanzania (BANK OF AFRIKA TANZANIA BOA), Bw. Ismail Said
Mohamed, kutoka Tawi la Benki hiyo Mtwara, ametangazwa leo kuwa mshindi wa gari mpya aina ya TOYOTA BREVIS, wakati wa
droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.
Wakati Bw.
Mohamaed akishinda gari hilo mpya kabisa, mteja menzake Thureiya Zabron Mgamba naye ameibuka
mshindi wa pili katika Promosheni hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya tawi la Benki hiyo
Kijitonyama, Jijini Dar es Salaam baada ya kushinda Pikipiki mpya aina ya TOYO.
Katika
mchezo huo wa Bahati Nasibu uliosimamiwa na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya
kubahatisha nchini, Bw. Mrisho Millao, washindi wengine watatu pia walishinda zawadi
mbalimbali zikiwemo Tshirt, Simu za kisasa na vocha za manunuzi.
Awali
akizungumza na waanndishi wa habari, kabla ya Promosheni hiyo, Meneja
Uendeshaji Biashara wa BOA, Bw. Wasia Mushi, amesema, lengo la Poromosheni hiyo
ni kuongeza hamasa kwa watanzania ili wakumbuke kujiwekea akiba, huku
akisisitiza kuwa kujiwekea akiba ndio utamaduni halisi wa kuelekea katika
mafanikio.
Bw. Mushi
amesema wakati wote wa Promosheni hiyo iliyofanyika nchi nzima, wateja zaidi ya
2000 wa Benki hiyo walishiriki na kushinda zawadi mbalimbali. “Tumefurahishwa
sana jinsi Promosheni hii ilivyopokelewa na wateja wetu, tumeongeza idadi ya
wateja pia kukuza amana kwa wateja wetu”, anasema Bw. Wasia.
Amesema
pamoja na Promosheni hiyo kufikia tamati, Benki ya Afrika bado inaendelea
kuwahimiza wateja kuweka akiba kwa ajili ya manufaa ya jamii na kuahidi kuwa
wamejipanga kutoa huduma za kisasa kwa wateja.
Bw. Wasia
amesema Benki ya Afrika Tanzania imejiikuwa ikijimalisha kwa kuwa na mtandao wa
matawi 20 nchi nzima, ambapo matawi kumi yako Jijini Dar es Salaam, wakati
matawi mengine yakiwa Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Mtibwa, Kahama,
Mbeya, Mtwara na Tunduma.
Meneja
Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi akiwaonyesha
waandishi wa habari gari mpya aina ya Toyota BREVIS lililotolewa na Benki hiyo
kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba
mwaka jana. Wengine ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel
Moya (kulia) na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.
Meneja
Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi akionyesha gari mpya aina ya Toyota BREVIS lililotolewa na Benki hiyo
kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba
mwaka jana. Wengine ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel
Moya (kulia) na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.
Gari aina ya
Toyota Brevis lililotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Droo ya mwisho ya
Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.
Comments
Post a Comment