MTOTO ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA 'WATANZANIA TUMSAIDIE'


Mtoto Darisa Kiboma (16), mkazi wa Mbamba-Bay, Nyasa, mkoani Ruvuma ambaye sasa angekuwa kidato cha pili au tatu, anaumwa kwa zaidi ya miaka kumi na mbili, akiwa na tatizo la kichwa kikubwa, anahitaji msaada wa haraka ili aweze kufanyiwa upasuaji. TUMSAIDIE.
Huyu ndiye Darisa Kiboma aliyezaliwa mwaka 1996, alianza kuvimba kichwa akiwa na umri wa miaka minne. siku zote amelala tu, anahitaji msaada haraka, kama umeguswa na tatizo lake tuwasiliane kwa 0754296253. TUMSAIDIE kiumbe mwenzetu.Mama Mzazi wa MtotoDarisa (aliyelala), Bi. Enne Kiboma (aliyeketi) wakiwa na Mwandishi Mwandamizi wa ZBC, Bi. Msangu Said, alipowatembelea kujua hali ya mtoto huyo, nyumbani kwao Mbamba-Bay, kando ya Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru