NSSF YAJITOSA KUONDOA AIBU YA SOKA LA TANZANIA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa michezo (Sports Academy) kitakachoanzishwa eneo la Kigamboni Dar es Salaam kwa ushirikiano wa NSSF na  Klabu ya Real Madrid ya Hispania. Kushoto ni Meneja Usalama wa NSSF, Ramadhani Nassib, Mtaalamu wa Uongozi na  Menejimenti ya michezo, Henry Tandau na Afisa Uwekezaji Mkuu wa NSSF, Tajudin Kamugisha (kulia).

...........................................................................................................

Hivi karibuni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilisaini mkataba na timu ya Real Madrid ya Hispania kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF- REAL MADRID Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji vyaa mpira wa miguu. Kituo hiki kitajengwa katika eneo la Mwasonga Kigamboni, Dar es Salaam na wataalamu kutoka Real Madrid watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 na 19 ili kukuza mchezo wa soka, kupata wachezaji bora wanaouzika nje na ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi Habari, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo utakuwa sehemu ya uwekezaji wa shirika hilo ulioanza baada ya kusaini mkataba. ambapo NSSF imeanza utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo utafutaji wa vipaji vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kila wilaya kwa Wilaya za mkoa wa Dar es salaam na utafanyika  kwenye viwanja vya Karume.

Dkt. Dau amesema zoezi hilo litakuwa linafanyika kati ya saa moja asubuhi hadi saa 9 alasiri  kwa tarehe zilizoainishwa. Amesema andikishaji washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi Februari 14 na 15, 22 na 23  mwaka huu na kufuatiwa na michezo ya majaribio Februari 28 na Machi moja, 2015 kwa wilaya  zote za Dar es salaam, ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF amesema, zoezi la uandikishaji halitafanywa kwa gharama na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika awamu mbili za dakika 30, kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao vya michezo.

Amesema Vijana 500 kati watakaofanyiwa majaribio wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 ambao ndio wataingia katika  shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza.

Dkt. Dau amebainisha kuwa wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi au walezi wao wakiwa na vitambulisho vyao, na kijana husika awe na Cheti  halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha mbili za pasport za rangi ya blue. Muda wa uandikishaji na majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.
Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri katika tasnia hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru