KASHESHE
VI
Ilikuwa saa
nne na nusu usiku, wakati Jean na kundi lake walipoondoka Kibumba kuelekea
Goma.
"Hakika
nimeridhika na ari ya wanajeshi wetu na uwezo mkubwa wa vikosi vyetu, pia
nimefurahishwa sana na aina ya silaha tulizonazo, hii inaonyesha ni jinsi gani
tumedhamilia kufanya kweli", Jean alisema kwa kujiamini.
"Nilikwambia
toka mwanzo kuwa ukifika na kuona lazima utaamua tuingie vitani, kwani hakuna
sababu wala haja ya kusubiri, vita vianze moja kwa moja, tuchukue madaraka",
Col. Gatabazi alitamba huku Jean akitingisha kichwa kukubaliana nae.
"Twendeni
Goma tukafanye maamuzi. Sijui kwa upande wa wenzangu, lakini mimi nafikiri
tuanze mashambulizi alfajiri na mapema ila kwanza tukamate vikosi vya hapa
Gisenyi kabla ya jua kuchomoza, maana adui hajui nguvu zetu, sisi nguvu yake
tunaijua", Jean alishauri, wote kwa pamoja wakakubaliana.
"Mimi
niko tayari wakati wowote, hata sasa vijana wangu wako tayari, uamuzi wenu tu ndio
unasubiliwa", Col. Gatabazi alijibu.
"Haya
twendeni Goma tukafanye uamuzi mara moja", Jean alijibu wakaondoka haraka kuelekea
Goma.
ITAENDELEA
0784296253
Comments
Post a Comment