MICHUANO YA NSSF MEDIA CUP 2015 MWANANCHI HOI KWA TUMAINI

Wachezaji wa Mwananchi Communication, Iman Makongoro (kulia) na Luth Liana wakiutamani mpira unaolindwa na Jesca Claud wa Tumaini Media, wakati mchezo wa awali wa netiboli wa NSSF MEDIA CUP 2015  kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe Dar es Salaam. Tumaini Media walishinda 14 -12.

Luth Liana (kulia) wa Mwananchi Communication na Jesca Claud wa Tumaini Media wakichuana vikali kuwania mpira wakati wa mchezo wa awali wa netiboli wa NSSF Media Cup 2015, uliochezwa kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe. Tumaini Media walishinda 14-12.

Kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, wachezaji wa netiboli walilazimika kuogelea kwenye madimbwi ya maji wakati wakiziwakilisha timu zao kusaka kombe la NSSF Media Cup 2015.

Lilian Timbuka wa Mwananchi akionyesha ishara ya kuomba ruhusa ya mwamuzi ili aweze kurusha mpira huku wachezaji wenzake wakimsubiri wakati wa mchezo wa awali wa netiboli kuwania kombe la NSSF Media Cup 2015

Lilian Timbuka wa Mwananchi Communication akiwa hoi uwanjani haamini macho yake baada ya timu yake kubugizwa na Tumaini Media mabao 14 -12

Iman  Makongoro wa Mwananchi akijiandaa kupokea mpira kutoka kwa Lilian Timbuka huku mchezaji wa Tumain Media Rose Michael akiwaangalia kwa makini.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru