MSHINDI ‘WEKA NA USHINDE’ AONDOKA NA GARI
Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo baada ya kukabidhi zawadi ya gari kwa Bw. Said Mohamed Bakari.
.....................................................................................................................................

NA MWANDISHI MAALUM, DAR ES SALAAMMshindi wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na Benki ya Afrika Tanzania (BOA Bank), Bw. Said Mohamed Bakari, ambaye ni mteja wa benki hiyo mkoani Mtwara, ameondoka Dar es Salaam leo akiwa anaendesha gari yake mpya aina ya  Toyota Brevis aliyoshinda.

Bw. Bakari ameondoka kwenye viwanja vya benki hiyo, Kijitonyama, Dar es Salaam akiendesha gari hilo mwenyewe, muda mfupi baada ya kukabidhiwa funguo za gari hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah watika wa hafla fupi iliyofanyika saa nne asubuhi leo.

Akizungumza kwa furaha baada ya kupokea funguo za hari hilo, Bw. Bakari (34) mfanyibiashara wa vifaa vya umeme mjini Mtwara, amesema pamoja na kupigiwa simu akifahamishwa kuwa mshindi wa promosheni ya ‘Weka na Ushinde, hakuamini kabisa kuwa ameshindia gari.

“Nilisikia kama ndoto za mchana, sikutegemea kama nikuja kumiliki gari nzuri kama hii, bado naona kama ndoto, nimefurahi sana kushinda na kupewa gari hii leo” alisema Bw. Bakari, alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam na akisisitiza kuwa amefurahi sana na kuishukuru BOA benki kwa kuendesha promosheni hiyo bila ujanja.

Amesema anaona fahari kubwa kuwa mteja wa BOA bank Tanzania na kwamba kitendo cha kushiriki Promosheni hiyo hakijamsaidia tu kwa kushinda gari, bali pia kimemsaidia kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

“Pamoja na kushinda zawadi hii kubwa, pia promosheni hii pia imenisaidia sana kuongeza bidii ya kujiwekea akiba benki, kitendo ambacho kitanisaidia sana katika shughuli zangu za kijamii na kiuchumi”, alisema na kuwaasa watanzania hususan wafanyabiashara wa aina zote kujijengea utamaduni wa kuweka akiba kwenye benki hiyo mara kwa mara ili waweze kushinda zawadi.

 Akizungumza baada ya kukabidhi gari hilo kwa mshindi, Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah amesema benki yake imefurahishwa sana na imani kubwa waliyonayo watanzania kwa benki hiyo  na kwamba hiyo imewafanya waongeze jitihada za kutoa huduma bora za kibenki zinazoendana na mazingira halisi ya soko la Tanzania.

Bw.  Ammish Owusu-Amoah amesema promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ ni moja ya hatua ya benki hiyo kujwashawishi watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba, kwani hilo ni suala la msingi sana kwa mtu kupata maendeleo kwa kujiwekea akiba.

“Tumekuwa hapa Tanzania kwa Zaidi ya miaka 10 Sasa na tunafurahi kuona kuwa tumechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa huduma za kibenki hapa nchini. Pia tumeanzisha huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zinawalenga wateja wetu wa kada mbalimbali za kimaisha na kiuchumi”, anasema Bw. Ammish na kuongeza kuwa ndani ya kipindi hicho, benki hiyo imefanikiwa kukua kwa kila Nyanja ikiwemo mtaji, idadi ya wateja pamoja na mtandao wa matawi yake.

Amesema kwa sasa BOA bank Tanzania ina mtandao wa matawi 21 ambapo 11 yapo jijini Dar es Salaam kikiwemo kituo cha kibiashara na mengine 9 yapo  Arusha, Mwanza, Kilimanjaro (Moshi), Morogoro (Morogoro Mjini na Mtibwa), Mbeya, Mtwara, Tunduma na Kahama.

Mkurugenzi huyo amesema benki yake ipo kwenye mchakato wa kufungua matawi mengine maeneo mbalimbali ya nchi ndani ya miezi sita.

Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ ilianza Octoba mwaka jana na takriban wateja 2,000 walishiriki huku wakijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo T- shirts, kofia, simu za mkononi, Tablets, Shopping Vouchers, na zawadi za juu ambazo ni Pikipiki na Gari aina ya Toyota Brevis.


Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah (kulia), akimkabidhi Bw. Said Mohamed Bakari, mfano wa funguo za gari aina ya Toyota Berevis, baada ya kushinda Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’ iliyoendeshwa na benki hiyo, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah (katikati), akiwa na funguo za gari hilo kabla ya kumkabidhi, mshindi wa ‘Weka na Ushinde’ Bw. Said Mohamed Bakari. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule.

Waandishi wa habari wakizungumza na
Huyu ndiye mshindi wa gari aina ya Toyota Brevis
, Bw. Said Mohamed Bakari.
Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah akijaribu kufunga mlango wa gari hilo baada ya kukabidhi funguo kwa mshindi wa promosheni ya ‘Weka na Ushinde’, Dar es Salaam leo.
Bw. Said Mohamed Bakari akiwapungia waandishi wa habari mkono wakati akiondoka.Mshindi wa pili wa Promosheni ya ‘Weka na Ushinde’, Bi. Rhoda Manase (aliyemwakilisha Bi. Thureiya Zabron) akipoke pikipiki kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa BOA bank Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah.

“Tumemaliza salama”, ndivyo wanavyosema Mkurugenzi Mtendaji wa BOA benk Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah na Ofisa Mwandamizi wa Benki hiyo, Bw. Solomon Haule, baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi leo

 


Comments

  1. Hi Nyakasagani,

    Unafanya kazi nzuri sana.
    Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa riwaya za zamani za musiba. Mbona hujapost tena episode inayofuata ya UCHU tangu ulipopost KASHESHE XIV?

    ReplyDelete

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru