WAZIRI CHIZA ATEMBELEA MIRADI YA NSSF DAR

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mataka, akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (kulia), kupita kwenye daraja la muda, alipotembelea miradi ya Uwekezaji inayofanywa na NSSF Dar es Salaam leo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (aliyeinua mkono), akiunyooshea kidole ukuta wa nyumba ambao mmiliki wake amegoma kuuvunja kupisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigambo, alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam leo. Wengine (mwenye suti nyeupe ni Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo, Mhandisi Karim Mataka na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (kulia).
Ujenzi ukiendelea kwa kasi katika Daraja la Kigamboni, linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ushirikiano na Serikali
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karim Mataka, akimwelekeza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (kulia), alipotembelea miradi ya Uwekezaji inayofanywa na NSSF Dar es Salaam leo. Wengine ni maofisa wa shirika hilo.


Mhandisi Karim Mataka akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mhandisi Christopher Chiza nguzo kumi na nne zinazolibeba daraja hilo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhandisi Christopher Chiza (aliyeinua mkono), akiangalia ramani za majengo alipofika kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba Kijichi.
Hizi ni baadhi ya nyumba zilizojengwa na NSSF kwa ajili ya kuuzwa
Hizi ni aina nyingine ya nyumba hizo zilizoko Kijichi, eneo la Kigamboni


Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU