NSSF YADHAMINI BONANZA :LA USALAMA WA AFYA MAHALI PA KAZI, YASAJILI WANACHAMA WAPYA

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Anthony Mavunde, akizungumza na wachezaji wa timu za Netiboli za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), wakati wa Bonanza la Usalama na Afya mahali pa kazi lililofanyika Dar es Salaam kwa udhamini wa NSSF.
 Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, akishiriki katika mchezo wa kufukuza kuku, wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa udhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Maofisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji, wakishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba, wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya hahali pa kazi lililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam juzi.
 Wafanyakazi wa OSHA wakishirimi mchezo wa kuvuta kamba
 Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakishangilia baada ya kutwaa kombe wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na kudhaminiwa na NSSF
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Mavunde, akimkabidhi, Nahodha wa NSSF, Pili Mogola, kombe la mshindi wa kwanza wa Netiboli, wakati wa Bonanza la Usalama na Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ali Chuo (kushoto), akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa timu ya Wizara ya Kazi, Abdallah Sanga, wakati wa Bonaza la Usalama na Afya mahali pa kazi lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa udhamini na NSSF
 Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, wakishiriki mbio za magunia wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya mahali pa kazi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (kulia) na Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, wakifanya mazoezi wakati wa maadhimisho ya Bonzanza la Usalama na Afya mahali pa kazi lililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaa


 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakishiriki katika zoezi la kujaza fomu za kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa ufadhili wa NSSF.
 Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Aysha Sango (kushoto), akikabidhi zawadi ya fulani kwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na shirika hilo, wakati wa Bonanza la Usalama wa Afya mahali pa kazi lililodhaminiwa na NSSF.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru