WAANDISHI WAMUAGA ELIZABETH MAYEMBA

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Habari za Michezo katika Gazeti la Majira, Marehemu Elizabeth Mayemba, likiwasili nyumbani kwake Tabata Kisukuru, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya misa takatifu na kuagwa na kusafirishwa kwenda Morogoro. kwa mazishi
 Mume na watoto wa Marehemu wakisubiri kuuaga mwili wa mpendwa wao Elizabeth Mayemba, aliyefariki Jumamosi, 
 Baadhi ya waandisshi wa habari na waombolezaji wakiandaa jeneza lenye mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba kwa ajili ya kumuaga rasmi nyumbani kwake Tabata Kisukuru leo.
 Wasemaji wa Klabu za Yanga na Simba, Jerry Muro (kushoto) na Haji Manara, wakitoa mkono wa pole kwa Mchungaji aliyeendesha ibada ya kuuga mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba, Hata hivyo wawili hao walitumia nafasi hiyo kutambiana. 
 Msemaji wa Klabu wa Simba, Haji Manara, akizungumza na waombolezaji, wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba.
 Msemaji wa Klabu Bingwa ya Tanzania, Dar Young Africans, Jerry Murro, akizungumza na waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba, nyumbani kwake Tabata Kisukuru leo.

 Msemaji wa Klabu ya Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani, iliyorejea Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, Masau Bwire, akijinafasi wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba
 Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA), Juma Abbas Pinto akisoma risala wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba.  

 Baadhi ya waandishi na waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa Mhariri wa Michezo wa gazeti la Majira, Marehemu Elizabeth Mayemba.
 Mwandishi wa habari za michezo katika gazeti la Nipashe, Somoe Ng'itu (kushoto) na wenzake wakilia kwa simanzi baada ya kuuona mwili wa Marehemu Elizabeth Mayemba, aliyeagwa Dar es Salaam leo. 
 Mwandishi wa Habari za michezo, Crala Alfonce, akiwa amezimia baada ya kuuona mwili wa rafiki yake Marehemu Elizabeth Mayemba.
 Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara (aliyevaa kofia) na Mwandishi wa Michezo, Saleh Ali, wakiteta jambo baada ya kuuaga mwili wa Elizabeth Mayemba.
Msemaji wa Yanga, Jerrt Murro (kushoto), akiteta na Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, baada ya kuuaga mwili wa Elizabeth Mayemba, nyumbani kwake Kisukuru, Dar es Salaam leo. Mwenye kofia nyeupe ni Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru