FARASHUU RATIBU, MCHEZA SOKA MWENYE NDOTO YA KUCHEZA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE

Farashuu Ratibu (pichani juu), msichana kinda wa miaka 19 mwenye ndoto ya kucheza soka katika timu ya Taifa ya wanawake Twiga Star, msichana huyu anacheza nafasi karibu zote za ushambuliaji. Lakini akisumbuliwa na tatizo moja tu, hasikii wala hawezi kusema. Mara ya kwanza kumuona katika viwanja vya Shule ya Sekondari Wazazi, iliyoko Ulongoni, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, akifanya mazoezi na timu za wanaume, nilivutiwa sana na kiwango chake awapo uwanjani. Nikapata taabu kidogo kuzungumza nae, lakini akawa mjanja kufikisha ujumbe kwangu. Haraka akapiga magoti na kuanza kuandika majina yake halisi, halafu akanieleza ndoto zake katika soka.

Farashuu anasema, alizaliwa mwaka 1997, Ulongoni, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alianza kucheza soka akiwa binti mdogo, hata akafanikiwa kucheza katika timu ya wasichana ya Msimbazi. Ni msichana mwenye kipaji cha soka, akiamini kuwa umri wake sasa unaruhusu kucheza soka katika timu yoyote itakayomhitaji.

Tofauti na wasichana wengine, Farashuu amekuwa gumzo mitaani hususan falsafa yake ya kupenda kucheza soka pamona na wanaume, akiwahi kufika mazoezini asubuhi, kukimbia na kucheza soka, akipiga mipira kwa mpangilio.

Anadokeza kwa kuandika chini kuwa anapata wakati mgumu sana uwanjani kwa vile hasikii wala hawezi kusema. Huku akibainisha kuwa mara nyingi anapokuwa na mpira, humwangalia zaidi mwamuzi wa mchezo iwapo atapuliza filimbi ya kuotea ama la.

 Farashuu akifanya mazoezi ya viungo
 Farashuu akikimbia wakati wa mazoezi

 Farashuu akiuchezea mpira wakati wa mazoezi

 Farashuu akiwa uwanjani, wakati akifanya mazoezi na timu ya wanaume, Ulongoni B


Farashuu akifanya vitu vyake uwanjani.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru