WILAYA MPYA YA KIBITI YAZINDULIWA MKOANI PWANI

 Maelfu ya wananchi wa mji wa Kibiti, Mkoani Pwani, wakiwa kwenye viwanja vya Stendi, mjini Kibiti juzi, kushuhudia makabidhiano ya Wilaya mpya ya Kibiti, iliyoanzishwa na Rais mwaka huu.
 Mkuu mpya wa Wilaya ya Kibiti, Gulam Shaban Hussein (kulia), akikabidhi madawati 537 yaliyotolewa na Serikali kwa Mbunge Jimbo la Kibiti, Ali Ungando kwa ajili ya Shule za Wilaya hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mkoani Pwani, Juma Njwayo (kulia), akikabidhi madawati 537 yaliyotolewa na Serikali kwa Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohammed Mchengerwa, kwa ajili ya Shule za Wilaya ya Rufiji. 
 Baadhi ya wananchi wakisubiri kushuhudia makabidhiano ya Wilaya mpya ya Kibiti.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mkoani Pwani Juma Njwayo (kushoto), akimtambulisha kwa wananchi Mkuu mpya wa Wilaya mpya ya Kibiti, Gulam Shaban Hussein, wakati wa sherehe ya kupokea Wilaya hiyo, kwenye viwanja vya Stendi Kibiti hivi karibuni. PICHA ZOTE NA SEIF NONGWA.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru