YANGA KUTUA LUBUMBASHI DRC JUMAPILI

Kikosi Yanga FC, kilichofungwa na Azam mchezo Ngao ya Jamii 

Na Mwandishi Maalum, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Dar es Salaam Yanga Afrika kitafanya mazoezi  ya mwisho Iumaa na Jumamosi kabla ya kushuka Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa Jumanne ijayo nchini humo.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa na mapumziko ya kutwa ya leo baada ya jana kupoteza mchezo kwa kufungwa kwa penalti 4-1 na wana lambalamba, Azam FC kufuatia sare ya 2-2 katika mchezo wa Ngao ya Jamii, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na sasa wanajiandaa kwa mchezo wa kukamilisha ratiba ya Kombe la Shirikisho wiki ijayo na wataondoka Dar es Salaam Jumapili.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezeshwa na refa Helder Martins De Carvalho wa Angola, atakayesaidiwa na washika vibendera Jean Claude Birumushashu wa Burundi na Arsenio Chadreque arengula wa Msumbiji. Maofisa wengine watakuwa, Antonio Muachihuissa Caxala wa Angola, Gerges Rodolphe Bibi kutoka Shelisheli, Ali Mohamed Ahmed wa Somalia na Russell Paul wa Afrika Kusini.

Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi 10 baada ya mechi tano na imefuzu hatua ya Nusu Fainali, ikifuatiwa na Medeama ya Ghana, yenye pointi nane, Mouloudia Olympique Bejaia pointi tano na Yanga inayoshika mkia kwa pointi nne. 
Medeama itahitaji sare Jumanne dhidi ya wenyeji Bejaia zitakapocheza nchini Algeria.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru