AJALI MBAYA YA MABASI YAUA ABIRIA WENGI


Taarifa za awali zinaarifu kutoka mkoani Mara kuwa Watu zaidi ya 60 wanadhaniwa kufariki dunia baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso mkoani humo muda mfupi uliopita. Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imesababishwa na  uzembe wa madereva wa mabasi hayo kutoheshimu sheria za Usalama Barabarani, kama inavyoonekana katika picha.

Ajali hiyo imehusisha basi ya J4 lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Tarime, mkoani Mwanza na basi la Mwanza Coach lililokuwa likitokea Musoma. Akielezea chanzo cha ajali hiyo, mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina amesema ajali hiyo ilitokea eneo la daraja huku kukiwa na bango kubwa linalosomeka Single line (yaani Njia Moja).

Amesema basi la J4 likiwa nyuma ya gari dogo aina ya Toyota LandCruiser lilijaribu kulipita gari hilo dogo bila tahadhari yoyote ndipo ghafla likakutana na basi la Mwanza Coach lililokuwa likisubiri magari ya upande wa pili yapite, Taarifa ambazo badi hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinasema zaidi ya maiti 60 zimenasuliwa kutoka kwenye mabaki ya mabasi hayo .
Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru