WANANCHI IKWIRIRI WAFUNDISHWA KUFUGA NYUKI

 Mtaalamu wa Nyuki, Bw. Avit Mtema (aliyesimama) akifungua mafunzo ya ufugaji nyuki wadogo (wasiouma) mjini Ikwiriri, Rufiji, Mkoani Pwani juzi, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wafugaji Nyuki Rufiji (RUFIJI BEEKEEPERS ASSOCIATION). Wengine kutoka kulia, Bi. Suzan Kisenga, Mussa Mlawa,Mawajabu Makarani na Bi. Fatma Mbuzi.  
 Mwezeshaji Bw. Mussa Mlawa (kulia), akimsikiliza kwa makini mtaalamu wa wa mizinga ya nyuki, Bw. Said Omary Shonvi wakati akielezea jinsi ya utengenezaji wa mizinga ya kisasa na vipimo vyake. 
Mtaalamu wa kutengeneza mizinga ya nyuki, Bw. Saidi Omary kutoka Mkuranga akiandaa mzinga wa kisasa na kuwaonyesha washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa nyuki wasiouma.  
 Washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa nyuki wasiouma wapanga vijiti ndani ya sanduku la kufugia nyuko ili kuweza kuingiza nyuki katika mzinga huo.  
 Muwezeshaji, Bw. Said Mlawa, akihamisha nyuki wasiouma kutoka kwenye mzinga wa zamani kuingiza kwenye mzinga wa kisasa. 
 Muwezeshaji Bw. Mussa Mlawa akigawa maziwa ya nyuki kwa washiriki wa mafunzo ya ufugaji nyuki.
 Bi. Suzan Kisenga akimkabidhi asali ya nyuki wasiouma Bw. Moshi Mtulia (MZEE KINYONGA) ili ichujwe kwa ajili ya matumizi.
 Bw. Ditrick Nyoni kutoka Mkuranga akipasua gogo lenye nyuki wasiouma kwa ajili ya kuhamisha kundi la nyuki wasiouma kutoka kwenye gogo hilo kwenda kwenye mzinga wa kisasa. 
 Muwezeshaji Bw. Mussa Mlawa, akihamisha kiota kutoka kwenye gogo kwa ajili ya kuingiza kwenye mzinga wa kisasa. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Tarafa ya Ikwiriri, akizunguza na washiriki wa mafunzo ya ufugaji nyuki. Wakati akiwaeleza faida za ufugaji nyuki wa kisasa.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU