YANGA, SIMBA WAPISHANA KWA PRISON MBEYAMICHEZO mitatu ya viporo vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya nane ya mzunguko wa kwanza, sasa zitafanyika kesho Jumatano. Simba ambao walikuwa wakijivunia kutofungwa katika ligi ya msimu huu wanakwenda Mbeya kuwakabiri Prison wakiwa na kidonda kibichi baada ya kuangukia pua mbele ya vijana wa African Lyon ya Dar es Salaam. 

Yanga ambao walifanikiwa kutibu majeraha ya kufungwa na Mbeya City, kisha kuibuka na ushindi mwembamba mbele ya Prison, wanakabiliwa na kibarua kingine kigumu Uwanja wa Uhuru, watakapocheza na vijana wa Masau Bwire, Ruvu Shooting, wakati huo huo Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam nazo zitachezwa kwenye Uwanja wa Mwadui, Awali pamoja na mechi hizo kuwekwa kwenye ratiba, lakini hazikuwa na tarehe huku ikielekezwa tarehe zitatajwa baadaye. 

Wachezaji wa Yanga walioibuka na ushindi mbele ya Prison (pichani juu) na Simba waliofungwa na African Lyon (chini), wanakabiliwa na mtihani mkubwa kesho, iwapo Makocha wa timu hizo, Hans Van Del Plujim wa Yanga na Joseph Omog wa Simba watawaamini tena vijana wao. Hata hivyo Azam nao wana kibarua kigumu zaidi ya kufungwa 2-0 na Mbao ya Mwanza. 

Ligi Kuu msimu huu imekuwa na ushindani mkali, ukiondoa wakongwe Yanga na Simba, ambao bado wanafukuzana kileleni, Simba wakiongoza kwa pointi 35 mbele ya Yanga wenye pointi 30. Stand United ambao walipanda Ligi Kuu msimu uliopita na kupona kushuka daraja msimu huu wamekomaa katika nafasi za juu, wakifundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Patrick Lewig.

Mbao ya Mwanza ndiyo timu pekee iliyopanda daraja msimu huu na kuonyesha makeke, ikiwa katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi. Hata hivyo wachambuzi wa masuala la Soka wanasema huo ni mwanzo mzuri kwa timu hiyo lakini isibweteke, kama zilivyofanya Pamba ya Mwanza na Tukuyu Stars ya Mbeya, ambazo zilionyesha ushindani wa muda .


Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru