KIKOSI CHA KISASI

SEHEMU YA TANO 

V

Ilikuwa saa saba kamili, Willy alipoingia ndani ya baa ya uwanja wa ndege wa Ndjili wa mjini Kinshasa, tayari kuwapokea akina Ozu. Ndani ya baa mlijaa watu wengi waliokuwa wakisubiri wageni wao. Willy aliamua kwenda kwenye kaunta ambapo aliagiza kinywaji. Ilipotimia saa saba unusu Robert naye aliingia ndani ya baa hii na alipomuona Willy alimfuata moja kwa moja.

"Vipi umeshafika huku?" Rbert alimuuliza Willy.

"Bila shaka nimefika ndiyo sababu niko huku". Alijibu Willy kimatani.

"Salama lakini?".

"Salama tu".

"Vipi ulifika kwenye mazishi?".

"Ndiyo nilifika, lakini watu walikuwa wengi mno sikukaa sana".

"Lo, kweli marehemu kazikwa kishujaa kweli kweli. maelfu ya wananchi wamehudhuria mazishi. Watu wamesema yalikuwa mazishi ya kihistoria."

"Hata mimi sijawahi kuona mazishi kama haya", alijibu Willy.

"Juu ya mambo yale uliyoniagiza jana. Marehemu alipewa gari lile asubuhi ya siku ile aliyouawa saa mbili hivi. Hili gari lilikuwa limetoka matengenezo siku hiyo hiyo."

"Gereji gani?". Aliuliza Willy kwa sauti nzito.

"Gereji moja iitwayo Papadimitriou, ambayo ni kati ya nyingi maarufu zinazotengeneza magari aina ya Peugeout hapa mjini Kinshasa".

"Una maana gari alilokuwa anatumia marehemu ilikuwa aina ya Peugeout?".

"Ndiyo ilikuwa Peugeout 504. Na inasemekana kuwa marehemu hakuwa ameliweka mahali popote kwa muda mrefu kiasi cha mtu kuweza kulifanyia mbinu za namna hiyo. Lakini ukifikiria teknolojia ilivyo kwa sasa hivi inaweza kumchukua mtu muda mfupi sana kutega bomu kwenye injini ya gari."

"Hii gereji ni ya nani?".

"Gereji hii ni ya Mpakistani mmoja tajiri sana aitwaye Papadimitrian. Ni mtu anayeheshimika sana hapa mjini, na ana mahusiano mazuri na Serikali, sababu magari mengi ya serikali yanatengenezwa kwake."

"Ni mzaliwa wa wapi?".

"Ni mzaliwa wa Pakistani, lakini ameingia hapa kwa kutokea Zambia ambako alikuwa akifanya biashara", Hata mimi nakumbuka kuwa alikuwa na duka kubwa sana la nguo mtaa wa Cairo mjini Lusaka. Yeye aliingia hapa mwaka 1968 na kabla ya kuwa na gereji hii alikuwa na duka kubwa la madawa huko Gombe mtaa wa Posta. Kwa ujumla ni mtu mwenye sifa nzuri na hana rekodi yoyote mbaya".

"Sikuwa na maana kuwa anaweza kuwa na ubaya, ila tu nilitaka kuwa na uhakika na gereji hii ni ya namna gani."

"Ni sawa kabisa kumtilia mashaka maana jambo hili lilipotokea hata mimi ilinibidi niwe na uhakika na gereji hii kabla sijaendelea popote." Mara walikatwa kauli na tangazo.

"Tafadhali sikilizeni, tunawatangazia kuwasili kwa ndege ZC 883 ya Shirika la Ndege la Nigeria itokayo Logos na kupitia na kisha kuelekea Librevile na kisha kuelekea Brazaville. Abiria wote wanaoondoka na ndege hiyo wanaombwa kuelekea kwenye chumba cha kuondokea. Asanteni.

"Hao wanaingia, je wewe unawafahamu?" aliuliza Robert. "Ndiyo, kwa picha. Wewe je?".

"Mimi siwafahamu ila nilifikiri kuwa utakuwa unawafahamu ndiyo sababu nimekuwahi." Waliondoka na kuelekea sehemu ya kuagiza 'waving bay', watu walikuwa wamejazana sehemu hii. Willy na Robert walijipenyeza na kuiangalia ndege hii ya aina ya DC 8 ikishuka taratibu.

ITAENDELEA 0784296253

Comments

Post a Comment

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU