Analog Clock

NSSF

NSSF
NSSF TANGAZO

Tone Radio Tz

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

Thursday, January 12, 2017

MKUTANO WA UCHAGUZI MKUU M.T.A JANUARY 16

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkutano Mkuu kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Wananchi wa Mkoa wa Mara waishio Dar es Salaam, cha Mara Twibuche Amacha (MTA), ambayo kwa kiswahili ni Mara tuamshane kwenye matatizo, umepangwa kufanyika January 16, 2017 katika Ukumbi wa Green Pub, ulioko Vingunguti, eneo la Relini, Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam. 
 Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya MTA, Bw. Godfrey Isomba Samaki (aliyeketi kushoto katika picha), Mkutano huo umepangwa kuanza majira ya saa sita mchana, amewataka watu wote wa mkoa wa Mara kufika kwa wingi siku hiyo kwa ajili ya kujadili mkutano huo muhimu wa uchaguzi.


Wajumbe wengine katika picha kutoka kulia ni Mwenyekiti wa zamani wa MTA. Bw. Musira Magoma Katende, Bw. Mbogo Nyakangara (Mkumbe), Bw. Samson Iganyega (Katibu wa Kamati) na Bw. Ali Magambo (Mjumbe. Kamati hii inayoundwa na watu kumi imekutana leo kwa ajili ya kupanga pamoja na mambo mengine sehemu ya mkutano huo.

Wajumbe wengine katika Kamati hiyo ni Bw. Nyakasagani Masenza (Mjumbe), Bw. Shaaban Athuman (Mjumbe), Bw. Jumanne Sukari (Mjumbe), Bw. Mwiburi Chamuriho (Mjumbe) na Bw. Mussa Mstapher (Mjumbe)


No comments:

Post a Comment