RAIS MAGUFULI ATANGAZA RASIMI VITA KWA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (pichani katika vazi la kivita), amewatangazia rasmi vita kali kwa wafanyabiashara hatari wa dawa za kulevya waliokuwa wameota mizizi mirefu na kufanya biashara hiyo wapendavyo. 

Akizungumza na vyombo mbali mbali vya habari, Ikulu Dar es Salaam, Rais Magufuli amevitaka vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kusimama imara kupigana vita hivyo ambayo ameahidi kuwa serikali itashinda. amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu kwa kusimama imara kupinga biashara hiyo pamoja na kuwepo vishawishi.

"Kazi yako nzuri sana Kamanda Mangu, wamekuwa wakikupigia simu na wewe umekataa kushiriki katika jambo hili, vinginevyo hata wewe leo usingekuwa IGP, wamekushawishi wameshindwa. Bahati nzuri vyombo vyote viko hapa, kazi hii si ya Makonda peke yake ni yetu watanzania wote", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amempongeza kwa dhati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kusimama imara kuanzisha vita dhidi ya watumiaji na wasambazani wa dawa za kulevya nchini. Amesema Serikali yake itasimama imara kuhakikisha biashara hii inakomeshwa kote nchini Tanzania.

Amevitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kupigana vita hivi, huku akiwataka Polisi kuwafikisha Mahakama haraka watu watakaobainika kufanya biashara hiyo. Amesisitiza kuwa dawa za kulevya ni hatari katika jamii hivyo watanzania wasiogope kupambana na mtandao huo.

"Mheshimiwa Kaimu Jaji Mkuu, hakikisheni kesi za watu wa unga mnazipeleka haraka haraka ili watu hawa wafungwe, msiwaogope kwa umaarufu wao, hata kama ni mke wangu Janeth kamata, mfano mmoja amekamatwa Lindi lakini sijui kwanini bado hajafikishwa makamani kujibu tuhuma", alisema,   


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akisisitiza jambo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimsikiliza kwa makini Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Wiliam Mkapa.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akikumbatiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU