MULTICHOICE KUTUNUKU WATEJA CHANELI ZA BURE


Kampuni ya Multichoice imetangaza kuanzisha programu mpya ya kutoa zawadi kwa kuwatuza wateja wake wa DStv kwa kuwaongezea chaneli mpya kwenye vifurushi vyao bila malipo yoyote ya ziada.

Programu hiyo ijulikanayo kama - DStv THANKS ilizinduliwa hivi karibuni mahsusi kwa ajili ya kuwashukuru wateja wake ambao wamekuwa wanatumia huduma za DStv kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi.

Wateja hawa watapata zawadi ya kuongezewa Chaneli nne mpya kwenye vifurushi vyao zikiwemo za tamthilia, sinema, elimu, sanaa na vichekesho. Chaneli hizo ni pamoja na ile maarufu ya sinema za kihindi ijulikanayo kwa jina la Zee Bollymovies itakayopatikana DStv chaneli 114. Chaneli hii itakuwa na sinema za kihindi za zamani pamoja na zile za kisasa kama vile Mohra, Kushi, na Fitoor.
Chaneli nyingine itakayotolewa kama zawadi kwa wateja ni Viasat Life itakayoonekana DStv chaneli 177. Hii imesheheni burudani, wasifu wa watu wa kawaida ambao waliweza kufanya mambo makubwa pamoja na mambo mengi ya maisha ya kila siku huku ikibeba vipindi kama vile Martha & Snoop’s Potluck Dinner Party, ‘The Rock’, Wake Up Call,  House of Curves, The Three Day Nanny na My Floating Home.

Nina TV itakayoonekana DStv chanel 143  ni maarufu kwa tamthilia zikiwemo zile za Kiafrika na za Amerika Kusini. Pia Chaneli ya Trigger itakayoonekana DStv chanel 188 nayo pia itatolewa kama sehemu ya zawadi kwa wateja wa DStv.

Kwa kuanzia Tarehe 7 hadi 21 mwezi huu, wateja wote wa DStv watapata chaneli hizo na baada ya hapo zitaendelea kubaki kwa wateja ambao wametumia mfululizo huduma za DStv kwa miezi mitatu na zaidi. Kila mteja anayefikisha miezi mitatu ya kutumia mfululizo huduma za DStv atakuwa anapata chaneli hizo za ziada bila akujali aina ya kifurushi anachotumia.

Akizungumzia programu hiyo ya kuwazawadia wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande amesema, “Tunafurahi sana kuzindua programu hii mahsusi ya kuwashukuru wateja wetu. Ni dhamira yetu endelevu kuwaheshimu na kuwathamini wateja wetu kwa dhati, hii ndiyo sababu kubwa inatufanya tuwape fursa hii adhimu ya kuweza kufurahia zaidi huduma zetu.” Alisema Maharage.

Aidha amesema kuwa Multichoice itaendelea kuhakikisha kuwa huduma za DStv zinaendelea kuboreshwa na kufikishwa kwa wananchi wengi zaidi ili waweze kufurahia maudhui yaliyomo kuanzia michezo, burudani, habari, elimu na hata chaneli za kidini pia.

Mkurugenzi huyo amesema mbali na kuwajali wateja wake, Multichoice pia itaendelea na programu zake nyingine za kijamii kwa lengo lile lile la kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini. Ameahidi kuwa mwaka 2017, Multichoice imejipanga kuendelea kushiriki katika kuimarisha michezo, taaluma na ubunifu.
Kampuni ya Multichoice Tanzania imekuwepo hapa nchini kwa takriban miaka 20 sasa na imekuwa kinara katika huduma za ving’amuzi ambapo king’amuzi chake cha DStv kimekuwa maarufu na kutumika kila pembe ya nchi hadi vijijini.Kwa maelezo tembelea  www.dstv.com/dstvthanks 

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU