SIMBA, MBEYA CITY HAPATOSHI TAIFA KESHO

LIGI Kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea  tena kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo vinara wa ligi hiyo vijana wa Msimbazi Simba (pichani juu) wanatarajiwa kushuka dimbani kuwakabili Mbeya City kutoka Mbeya kwenye huo.

Pamoja na mchezo huo, michezo mingine ya kesho Jumamosi Machi 4, mwaka huu, mahasimu wengine watakutana katika soka Toto Africans na Mbao FC za Mwanza zitakamatana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Simba wanashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono uliowawezesha kurejea kileleni baada ya kuwafunga wapinzani wao wa jadi Yanga 2-0 na kurejesha utulivu Msimbazi.

Katika mchezo huo, itawalazimu Simba kucheza kwa tahadhali kubwa kwani matokeo ya sare au kufungwa yanaweza kuwarejesha tena nafasi ya pili iwapo wapinzani wao Yanga watashinda mchezo wa Jumapili dhidi ya Mtibwa utakaopigwa mkoani Morogoro. 

Viongozi mbali mbali wa Simba wamejinasibu kushinda mchezo huo ikiwa ni falsafa yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu baada ya kuukosa kwa miaka kadhaa. 

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru