ALPHONCE SIMBU WA TANZANIA ATUA LONDON

Dar es Salaam, Aprili 20, 2017;  Mwanariadha pekee wa Tanzania Alphonce Simbu (pichani kulia), anayeshiriki mbio za London Marathon zitakazofanyika jijini London Jumapili ya wiki hii, amewasili salama Nchini Uingereza akiwa na ari kubwa ya kushiriki mbio hizo zinazotarajiwa kushirikisha wanariadha mashuhuri kutoka nchi mbalimbali duniani.

Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kuwapa wakati mgumu baadhi ya wanariadha nguli ulimwenguni wanaoshiriki mbio za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekela pamoja wa wengine kutoka Ethiopia na Kenya.

Akiongea muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kuelekea Uingereza, Simbu amesema amejiandaa kupambana kufa na kupona kuhakikisha kuwa ananyakua medali kwenye mashindano hayo. “Nitapambana kwa nguvu zangu zote. Ninakwenda London nikijua wazi kuwa naiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano haya makubwa. Nakwenda kupeperusha bendera ya Tanzania” alisema simbu na kuongeza kuwa “Nina imani nitashinda kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nina ari na moyo wa kushinda. Naomba sala za watanzania wote ili niweze kuleta medali nyumbani”.

Ameishukuru kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia King’amuzi cha DStv kwa kumdhamini na kuhakikisha anakaa kambini kwa muda wote huo bila shida yoyote. “Nawashukuru sana DStv kwa udhamini wao mkubwa wa kambi yangu ya mazoezi pamoja na mahitaji yangu mengine kwa kipindi kirefu sasa. Kwa kweli wao ndiyo waliofanikisha maandalizi yangu” Simbu amewashukuru pia wadau wote wa riadha hususan Chama Cha Riadha Tanzania pamoja na wizara inayohusika na michezo kwa jitihada zao za kuahakikisha safari yake ya kwenda London inafanikiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema kuwa wana imani kubwa na Simbu kutokana na mazoezi aliyofanya. “Tunafurahi kuwa baada ya kuweka nguvu kubwa sasa Simbu anakwenda kushiriki mashindano haya akiwa amejiandaa vizuri. Tunaamini atashinda, na pia huu ni mwanzo wa ndoto yetu kubwa, ya kusikia kwa mara ya kwanza wimbo wetu wa Taifa ukipigwa kwenye mashindano ya Olympic. Kwa mwenendo wake, tunaamin Simbu atatufikisha huko” alisema Maharage.

Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika jijini London mwezi wa nane mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016 ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi.

Alphonce anatarajiwa kurejea nchini Jumatatu Aprili 24 saa mbili asubuhi katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.


About Alphonce Felix Simbu;
Personal best: 2:09.21- Lake Biwa Marathon – Japan.

Born in Singida in 1992, Alphonce Simbu is a DStv ambassador and the latest Tanzanian International Gold Medallists.
2011: Alphonce was selected to represent Tanzania in All Africa Games in Maputo Mozambique after winning the 10,000m at National athletics Championship.
2012-2013: Alphonce trained and participated in different races as an invitee both within and outside Tanzania. 
2014: He was selected to join the national team for commonwealth Games held in Glasgow Scotland
2015: Participated in World Cross-country Championships in Gyuiyaang China.

It was on 6th July 2015 when Alphonce participated in his First Marathon race in Gold Cost and scooped 6th position recording a decent timing of 2:12.01. He then qualified for the IAAF 2015 Beijing World Athletics Championships one of the toughest races in the world. Against all odds, he emerged 12th. This gave him a global rating - the IAAF Gold label which qualified him for the 2016 Rio   Olympic Games. 

On 6th March 2016 He was honoured an invitation for the Lake Biwa Marathon in Japan grabbing 3rd position with a pleasant timing of 2:09.21. During the 2016: Rio Olympic Games, Alphonce further enhanced his record by recording 2:11.05 and making Tanzania proud by clutching 5th position.

His dream of winning a gold medal came true in 2017 when he won yet another highly contested International Marathon – The Standard Chartered Mumbai Marathon while reducing further his timing to 2:09:28!

Now Alphonce is a member of Tanzania National Team for the 2017 London IAAF World Athletics Championship to be held in London on 23rd August.

Association with DStv

In 2016 Multichoice Tanzania through its DStv service decided to invest in Athletics by sponsoring Alphonce Simbu in order to make sure he realise his dream of becoming a Gold Medalist. The company entered into a contract to support Alphonce Simbu for an initial period of one year to enable him to prepare well for the 2017 IAAF World Athletic Championship.

Multichoice provide Alphonce with subsistence allowance as well as financing his training. Currently Multichoice is fully sponsoring his training for the preparation of the upcoming London Marathon taking place on 23rd April 2017.
Multichoice Tanzania is supporting Alphonce as part of its Social Value Initiative of nurturing local talents.
For inquiries contact

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU