POLISI WALIOUA NA MAGAIDI PWANI WAAGWA DAR

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mwigulu Nchemba, akizungumza na wananchi kwenye Viwanja vya Polisi Kilwa Road, wakati wa kuuaga miili nane ya waliokuwa Askari wa Polisi, waliouawa na watu wanaodhaniwa kuwa Magaidi, huko Mkuranga, mkoa wa Pwani April 12 mwaka huu.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru, akizungumza na Askari na Wananchi waliofika kwenye viwanja vya Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam, wakati wa kuaga miili waliokuwa Askari wanane wa Jeshi la Polisi, waliouawa huko Mkuranga, mkoani Pwani April 12 mwaka huu. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Askari na Wananchi waliofika kwenye viwanja vya Polisi Kilwa Road, Dar es Salaam, wakati wa kuaga miili waliokuwa Askari wanane wa Jeshi la Polisi, waliouawa huko Mkuranga, mkoani Pwani April 12 mwaka huu. 
 Baadhi ya Askari wakiwa wamebeba miili ya waliokuwa Askari wenzao, waliouawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa Magaidi.
  Baadhi ya Askari wakiwa wamebeba miili ya waliokuwa Askari wenzao, waliouawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa Magaidi.
 Baadhi ya Makamanda wa Polisi, kutoka Idara mbalimbali za Jeshi hilo, wakiangalia kwa uchungu majeneza yaliyohifadhi miili ya Askari wanane waliouawa huko Mkuranga, Pwani.
 Kamanda Polisi Kikosi cha USalama Barabarani, Kamishna Mohamed Mpinga, akiangalia
 Baadhi ya Askari Polisi na wananchi wakiwaombea dua askari wenzao waliouawa baada ya miili yao kufikishwa kwenye Viwanja vya Polisi Kilwa Road kwa ajili ya kuagwa rasmi leo.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru, aliyeifuata miili ya askari hao waliotoka Morogoro, akiangalia saa kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani humo ambako wataagwa na kusafirishwa tena kupelekwa mikoa husika ikiwemo Mara na Arusha.
 Majeneza yenye miili ya askari hao.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mwigulu Nchemba, akiangalia kwa uchungu majeneza yenye miili ya Askari waliouawa.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mwigulu Nchemba (kushoto) akiongoza waombeleza kuaga miili ya Askari hao.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Brigedia Jenerali, Projest Rwegasira, akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yaliyohifadhi miili ya Askari wanane waliouawa mkoani Pwani juzi  
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru, akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yaliyohifadhi miili ya Askari wanane waliouawa mkoani Pwani juzi 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yaliyohifadhi miili ya Askari wanane waliouawa mkoani Pwani juzi na kuagwa Dar es Salaam leo. 
 Wakisalimia baadhi ya waombolezaji.
Askari wakipeleka miili hiyo kwenye magari kwa ajili ya kuelekea Morogoro.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru