MAKAMU RAIS AWASILI ARUSHA KUWAAGA WATOTO

Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan (pichani kushoo) amewasili Jijini Arusha asubuhi hii kwa ajili ya kushiriki kuwaaga wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa basi ndogo la Shule ya Lucky Vicent waliopata ajali mbaya ya barabara na kupoteza maisha huko Wilayani Karatu, Arusha Kaskazini mwa Tanzania, ambapo basi hilo aina ya Toyota Coster mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la Morombo, lilitumbukia katika Mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, Karatu kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, kilomita 160 kutoka mjini Arusha.

Vyombo mbalimbali vya habari, Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali na watu binafsi wameelezea kuguswa na msiba huu mkubwa kwa Taifa hivyo Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan atawakilisha watanzania wengine katika msiba huo mzito.  

Wanafunzi hao walikuwa wamebakiza kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea. Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na waalimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano. Mwandishi wa BBC mjini Arusha Ally Shemdoe, alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua inayoendelea kunyesha katika eneo hilo. 

Mwandishi huyo anasema dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyo alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni katika mto Malera. Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.

Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa mujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo, miili 32 ya watoto hao ilipelekwa katika hospitali hiyo, wakiwemo waalimu wawili na dereva.
Wakazi wa eneo la Karatu wakijaribu kuitoa miili ya marehemu hao baada ya kutokea kwa ajali hiyo mbaya
Hapa ni Shule ya Lucky Vicent, iliyoko Arusha.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru