BALOZI ABDUL CISCO MTIRO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Itifaki wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Wiliam Mkapa, Balozi Cisco Mtiro (pichani kulia) amefariki leo kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amina. 

Taarifa za kifo cha Mwana Itifaki huyo maarufu Cisco Mtiro, zimethibitishwa na Madaktari wa Hospitali hiyo na kuanza kusambazwa haraka na mitandao ya kijamii. Marehemu Cisco Mtiro anakumbukwa kuwa mtu pekee akuyyechuana vikali na aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. Agustine Mrema wakati wakiwania Ubunge wa katika Jimbo la Temeke.

Cisco aliyekuwa akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliifanya Temeke kuwa moto, baada ya viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kuendesha kampeni la kuhakikisha anaingia mjengoni lakini walishindwa.

Viongozi waliofika Temeke kufanya kampeni wakati huo ni pamoja na aliyekuwa Rais wakati huo Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu wakati huo Fredrick Sumaye, Katibu Mkuu Philip Mangula na wengine wengi wenye ushawishi katika siasi za Tanzania.

Pamoja na msukumo huo mkubwa, Mrema ambaye wakati huo nyota yake ilikuwa iking'aa aliwabwaga wakubwa hao maarufu katika serikali kuwa mbunge wa Temeke. Mtu anayetajwa kuwa chachu ya ushindi wa Mrema ni Mzee Mtopea. 

PUMZIKA KWA AMAN KAMANDA ABDUL CISCO MTIRO


Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU