IGP SIMON SIRO AANZA KAZI RASMI

Wiki moja baada ya kuapishwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro  (pichani juu kushoto), jana June 6, 2017, alifanya ziara ya kwanza katika Wilaya za Kibiti na Mkuranga kutimiza ahadi baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo. Eneo hilo la Pwani ni miongoni mwa maeneo ambayo mauaji yameripotiwa.

Mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo (IGP), Simon sirro aliahidi kutoa sh.milion 10 kwa atakayetoa taarifa za kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya viongozi huko Kibiti wilayani Rufiji, hususan Utete mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro alisema kumekuwa na mauaji ya wananchi na Askari katika Wilaya ya Rufiji katika eneo la Utete na Wilaya ya Mkuranga ambayo yamekuwa yakifanywa na wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao, 

Ameahidi kutumia muda mfupi kumaliza vitendo vya uhalifu na mauaji ya kutumia silaha yanayoendelea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani ambapo amesisitiza kushirikiana na wananchi kumaliza tatizo hilo.

Siro ambaye awali alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amesisisitiza utii wa sheria bila shuruti, hususan kwa waendesha bodaboda na raia wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wenzao.

Akasema Jeshi la Polisi bado linaendelea na Operesheni mbalimbali kuhakikisha kwamba vitendo hivyo haviendelei katika maeneo hayo. Aidha Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amezungumzia juu ya waendesha boda boda kuwa na tabia ya kukaidi kufata sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja ‘mishikaki.

Amesema waendesha bodaboda wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kupita taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu ‘Helment’ ambapo kumesababisha wengine vifo na majeruhi ya kuwafanya kuwa na ulemavu wa kudumu

Hata hivyo amesema kumekuwa na malalalamiko dhidi ya baadhi ya Askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa lakini pia baadhi ya wananchi kuwashawishi Askari kupokea rushwa ikiwa ni sehemu ya ngao ya kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa wamefanya makosa.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU