WATANZANIA WAMLILIA NDESA PESA

Salaam nyingi za rambirambi zinaendelea kutolewa kwa familia ya Marehemu Mzee Philimon Ndesamburo Kiwelu 'Pesa' Kwa wanae, hususan Lucy Owenya Kwa kumpoteleza baba yake mzazi. Ni msiba mkubwa Kwa watanzania hususan  Kilimanjaro na mji wa Moshi ambapo Mzee Ndesa Pesa alikuwa mwakilishi wao Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015. "Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote".

Ni msiba mkubwa Kwa wanachama wa CHADEMA ambao alikuwa Mwenyekiti wao wa Mkoa tangu Chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta. Huwezi kutaja maendeleo ya CHADEMA kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la Mzee Ndesamburo. Waliopata bahati ya kufanya naye kazi kwa karibu, wanaweza kutamka bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda Chama chake Kwa dhati Kabisa. Ni msiba mkubwa kwa Watanzania. Mzee Ndesamburo alitumia uwezo wake wa kifedha na kiakili kuimarisha mfumo wa Vyama vingi nchini kwetu. Wameeleza baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa nchini.

Mchango wake katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano na Kwa Kweli wengi wetu Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Mzee Ndesamburo na wenzake walio hai na waliotangulia mbele ya haki walifanya. Mzee Ndesamburo amechangia Sana ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Kupitia kampuni zake za Keys Hotels ameweza kuchangia Sana ukuaji wa sekta ya Utalii nchini kwetu. Bungeni alikuwa mstari wa mbele kutaka uhifadhi wa mlima Kilimanjaro kutokana na tishio la theluji kuondoka katika uhai wetu ( in our life time). Kwa hakika Vyuo Vikuu vyetu vya Umma vingekuwa vinatenda haki Mzee Huyu angepewa Shahada ya Uzamivu ya Heshima Kwa mchango wake katika Maendeleo ya sekta ya Utalii nchini kwetu. Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ‘ legacy ‘ yake. Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye mtihani huu mkubwa. Muwe wamoja na mshikamane. Poleni Sana ndugu zangu wa CHADEMA Kwa kupotelewa na Kiongozi wenu na Kiongozi wetu pia. Poleni Sana wana Moshi Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania. Pumzika Kwa Amani Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina

Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU