RIADHA WA WATANZANIA WAAHIDI MEDALI LONDON

Balozi maalum wa DStv na mmoja ya wanariadha wa Tanzania wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka 2017 yatakayofanyika mwezi 
ujao Jijini London, Alphonce Simbu, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani imejiandaa vizuri tofauti na miaka ya nyuma ambapo maandalizi yalikuwa hafifu.

Akizunngumza wakati wa ziara maalum ya Afisa muandamizi wa DStv Johnson Mshana (kama anavyoonekana katika picha kushoto) akiwa kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Ilboru, mkoani Arusha ambapo alishuhudia mazoezi ya timu hiyo, Simbu (wa tatu kulia) alisema yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanaleta medali katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika mwezi Agosti. 

Balozi huyo maalum wa DStv na moja ya wanariadha wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka huu yatakayofanyika Jijini London, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani imejiandaa vizuri

Pamoja na kuzunngumza na wanariadha Afisa huyo wa DStv Johnson Mshana alishuhudia mazoezi ya timu hiyo,  “Tumejiandaa vizuri na tunamatumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi mazito na inaonekana vijana tuko sawasawa kupambana katika mashindano hayo” alisema Simbu

Mshana ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania baada ya kutembelea kambi hiyo ameeleza kufurahishwa sana na mwenendo wa kambi na timu nzima. “Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi ya timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii ndiyo sababu iliyotusukuma DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya Taifa itakayokwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania tushuhudie medali zikija nyumbani” amesisitiza.

Amesema baada ya DStv kuanza kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita, wameshuhudia mafanikio makubwa sana. Ambayo yamewatia moyo na kuamua kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi timu ili hatimaye iweze kufanya vizuri zaidi na kulikwakilisha vyema taifa kwenye michuano ya kimataifa.

“Tulianza na Simbu, amefanya vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi kwa timu yetu ya Tanzania na tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv ilionyesha mubashara Mumbai Marathon tukamuona Simbu akishinda, Tukaonyesha Mubashara London Marathon, tukaona Simbu akivunja rekodi yake, na 
tutaonyesha mubashara Mashindano ya Dunia Mwezi Agosti, ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua medali kedekede na kuliletea taifa letu sifa kubwa” alisema Mshana kwa kujiamini

Naye Kocha wa timu hiyo Francis John, amesema kazi kubwa imefanywa na makocha wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kuna ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi yao kwenda vizuri. Amesema jumla ya wachezaji saba wakiwemo wanawake watatu na wanaume wanne ambao ni Failuna Abdi mita 10,000 Gabriel Gerald mita 5,000. Watano watashiriki marathon kamili ya kilomita 42 ambao ni Magdalena Krispin, Saraah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba na Alphonce Felix Simbu.

Timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo inatarajiwa kuagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa Jijini Dar es Salaam Julai 31 na Mashindano hayo yanatarajiwa kuaanza Augost 4, 2017.


 Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (kushoto) akiwa na wanariadha wenzake Nelson Mbuya (wa pili kushoto), Stephano Huche na Joseph Panga (kulia) wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Agost 4 jijini London
  Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake wakiendelea na mazoezi makali kwa ajili ya safari ya London
 Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Johnson Mshana (kushoto) akimkabidhi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (kulia) vifaa vya mazoezi wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya riadha Jijini Arusha.

 Balozi wa DStv Alphonce Simbu (kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake wa timu ya taifa itakayoshiriki Mashindano ya Riadha ya Dunia jijini London wiki ijayo Ezekiel Ng’imba (katikati) na Said Makula wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru